bayyinaat

Published time: 19 ,April ,2018      11:28:19
inapaswa Mwislamu awe ni mwenye kudhibiti nafsi yake mwenyewe kujihusisha na kazi yake (yanayo muhusu)- yaani ajichunge na kutekeleza majukumu yake mwenyewe ipasavyo na awatambue watu wa zama zake
News ID: 293


امام رضا(عں) في حكمة ال داود: ينبغ للمسلم ان يكون مالكالنفسه،مقبلا، على شأنه، عارفا باهل زمانه. ( اصول الكاف ج/ 224

Imamu Ali bin Mussa Alridha (a.s) amesema ya kwamba, amesema Abu ja'afar (a.s);

Imekuja katika hekima ya Aali-Daudi kwamba:

inapaswa Mwislamu awe ni mwenye kudhibiti nafsi yake mwenyewe kujihusisha na kazi yake (yanayo muhusu)- yaani ajichunge na kutekeleza majukumu yake mwenyewe ipasavyo na awatambue watu wa zama zake(na aamiliane nao kwa muamala kwa kadri anavowajua).

Katika maneno haya ya Imamu (a.s) kumeashiriwa maudhui tatu muhimu:

1- kujizuia na kudhibiti matakwa. Jambo hili ni msingi wakila malezi na maadili ya mwanadamu:

2- Mtu kuahidi kufungamana na nafsi yake ambayo ni njia ya kjijenga na njia muafaka ya kukuza kipawa cha mtu alicho nacho na maandalizi na nguvu za kipaji alizonazo mtu.

3- kutambua zama. Kwa hakika kutambua zama humuandalia mtu uwanja wa kuwatambua watu, matukio yanayojiri katika zama zake, humfanya aishi akiwa na uelewa kamili na hivyo huwa na usimamizi kamili wa kimantiki kwa migogoro.

Kwa utaratibu huu, ni jambo la dharura, kwa watu kutambua zama na kugundua sifa za kila zama, kuelewa mabadiliko ya kitamaduni, kiuchumi kisiasa n.k.

Watu wanapaswa kutambua kulingana na uwepo wao, zama na mazingira ya kijografia, ili ufahamu kuhusiana na watu hao uwe wa kina zaidi na kwa msingi huo kuishi nao iwe ni jambo jepesi na wakati huo huo, kua na mafungamano na mielekeo na watu hao liwe ni jambo ambalo lina msingi zaidi.

Allah atujalie tuwe ni wenye kuamiliana na watu kwa kuangalia zama husika.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: