bayyinaat

Published time: 22 ,April ,2018      20:21:53
News ID: 304

Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kujiri kwa mazungumzo baina ya Viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani, serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeutaka ulimwengu kwa ujumla kutambua madhara ya kukubaliana na Marekani katika jambo lolote.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo ambapo yupo nchini Marekani katika kuhudhuria mikutano ya Kimataifa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Marekani Bw Donald Trump kutangaza kwamba mpaka kufikia May 12 mwaka huu, itajulikana kwamba atapitisha makubaliano ya Iran na nchi sita kubwa juu ya Nyuklia au la, ambapo Iran imesema kwamba endapo Trump ataamua kuachana na makubaliano hayo basi ajiandae kukutana na radiamali isiyopendeza.

".....Ni hali ya hatari sana ambayo ningependa nchi yangu pamoja na ulimwengu kwa ujumla zitambue, kwamba hutakiwi kabisa kukualiana jambo na Marekani, kwa sababu mwisho wa siku kanuni ya Marekani ni kwamba changu ni changu na chako inabidi tukijadili....” Zarif Waziri wa mambo ya nje wa Iran alisema.

Pia katika mazungumzo yake hayo Bw Zarif amezionya nchi za Ufaransa pamoja na Ujerumani na kuziambia kwamba kitendo cha viongozi wao kujitahidi kumridhisha na kumfurahisha Bw Trump katika maamuzi yake ni kitendo ambacho hakiwezi kuzaa matunda yeyote.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: