bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      11:58:51
Moja ya madhambi makubwa, ambayo ameweka wazi Imamu Sadiq na Imam Kadhim na Imam Ridhaa pamoja na Imam Jawaad katika maneno yao ni kuvunja undugu, na zimekuja kemeo kali kutoka ndani ya Qur’ani tukufu..........
News ID: 327

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Moja ya madhambi makubwa, ambayo ameweka wazi Imamu Sadiq na Imam Kadhim na Imam Ridhaa pamoja na Imam Jawaad katika maneno yao ni kuvunja undugu, na zimekuja kemeo kali kutoka ndani ya Qur’ani tukufu na zimepokelewa laana juu ya tabia hiyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Pia imepokelewa kutoka kwa Imam Sajjad (a.s) kuwa amesema: "Epuka kusuhubiana na mvunjaji undugu, kwani nimemkuta amelaaniwa katika sehemu tatu ndani ya Qur’ani tukufu”.

1. Katika Surat al – baqara aliposema Mwenyezi Mungu:

"الَّذِينَ ينْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يوصَلَ وَيفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ أُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ".

"Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara”.[1]

Hutumika tafsida ya waliopata khasara ndani ya Qur’ani kuwa ni yule atakae adhibiwa siku akhera, ni kwa mujibu wa uthibitisho wa Aya mbili ambazo zitakujia hapo mbele zitujulishazo ya kwamba mvunjaji undugu amelaaniwa.

2. Anasema (s.w.t) katika surat al- Ra’d:

" وَالَّذِينَ ينْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يوصَلَ وَيفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ أُولَئِكَ لَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ".

"Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya”.[2]

3. Anasema aliyetukuka katika Sural Muhammad:

" فَهَلْ عَسَيتُمْ إِنْ تَوَلَّيتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ. أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ".

"Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?. Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao”.[3]

KUVUNJA UNDUGU KATIKA RIWAYA:

Hakika riwaya zithibitishazo maudhui hii ni nyingi mno ambapo hapa tutaashiria baadhi:

Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w):

" أَلَا إِنَ‏ فِي‏ التَّبَاغُضِ‏ الْحَالِقَةَ لَا أَعْنِي حَالِقَةَ الشَّعْرِ وَ لَكِنْ حَالِقَةَ الدِّينِ ".

"Tambua ya kuwa katika chuki lipo fundo kubwa, simaanishi fundo la nywele bali ni fundo lizuialo maendeleo ya dini”.[4]

Na imepokelewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s):

" اتَّقُوا الْحَالِقَةَ فَإِنَّهَا تُمِيتُ الرِّجَالَ قُلْتُ وَ مَا الْحَالِقَةُ قَالَ قَطِيعَةُ الرَّحِم ".

"Ogopeni fundo ya rohoni, kwani huwafisha watu wengi, nikamuuliza: ni lipi fundo hilo? Akasema: ni kuvunja undugu kwa kinyongo kilichoko moyoni”.[5]

AMALI MBAYA MNO MBELE ZA MUNGU:

Mtu mmoja alimjia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akamuuliza:

"أَنَّ رَجُلًا جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ ص فَقَالَ أَخْبِرْنِي مَا أَفْضَلُ الْأَعْمَالِ فَقَالَ الْإِيمَانُ بِاللَّهِ قَالَ ثُمَّ مَا ذَا قَالَ صِلَةُ الرَّحِمِ قَالَ ثُمَّ مَا ذَا قَالَ الْأَمْرُ بِالْمَعْرُوفِ وَ النَّهْيُ عَنِ الْمُنْكَرِ قَالَ الرَّجُلُ وَ أَيُ‏ الْأَعْمَالِ‏ أَبْغَضُ‏ مِنْهَا قَالَ الشِّرْكُ بِاللَّهِ ثُمَّ مَا ذَا قَالَ قَطِيعَةُ الرَّحِمِ قَالَ ثُمَّ مَا ذَا قَالَ الْأَمْرُ بِالْمُنْكَرِ وَ النَّهْيُ عَنِ الْمَعْرُوف".

"Ni amali ipi mbaya mno mbele za Mungu, akasema: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, akauliza: kisha kipi kingine: akasema: Kuvunja undugu: kisha kipi kingine: akasema: Kuamrisha mabaya na kukemea mema”.[6]

KUTENDA HISANI KWA NDUGU KWA KULIPIZA UBAYA:

Mtu mmoja alimshitakia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu adha ya jamaa zake wa karibu, akasema (s.a.w.w):

"جَاءَ رَجُلٌ فَشَكَا إِلَى أَبِي عَبْدِ اللَّهِ ع أَقَارِبَهُ فَقَالَ لَهُ اكْظِمْ‏ غَيْظَكَ‏ وَ افْعَلْ فَقَالَ إِنَّهُمْ يَفْعَلُونَ وَ يَفْعَلُونَ فَقَالَ أَ تُرِيدُ أَنْ تَكُونَ مِثْلَهُمْ فَلَا يَنْظُرَ اللَّهُ إِلَيْكُم".

"Dhibiti ghadhabu zako na tenda wema, akasema: Wao wanatenda mabaya na wanazidi kutenda mabaya, akasema (s.a.w.w): Je: wapenda kuwa mithili yao, basi tambua ya kwamba hatokutazama mwenyezi Mungu kwa jicho la huruma”.[7]

Kutoka kwa Imam Baqir (a.s) amesema:

" أَعُوذُ بِاللَّهِ‏ مِنَ‏ الذُّنُوبِ‏ الَّتِي تُعَجِّلُ الْفَنَاءَ فَقَامَ إِلَيْهِ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْكَوَّاءِ الْيَشْكُرِيُ‏ فَقَالَ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ أَ وَ تَكُونُ ذُنُوب‏ تُعَجِّلُ الْفَنَاءَ فَقَالَ نَعَمْ وَيْلَكَ قَطِيعَةُ الرَّحِمِ إِنَّ أَهْلَ الْبَيْتِ لَيَجْتَمِعُونَ وَ يَتَوَاسَوْنَ وَ هُمْ فَجَرَةٌ فَيَرْزُقُهُمُ اللَّهُ وَ إِنَّ أَهْلَ الْبَيْتِ لَيَتَفَرَّقُونَ وَ يَقْطَعُ بَعْضُهُمْ بَعْضاً فَيَحْرِمُهُمُ اللَّهُ وَ هُمْ أَتْقِيَاء".

"Mambo matatu hafi mwenyewe hata atapata natija yake, uonevu, na kuvunja undugu na kula yamini ya uongo”.[8]

Itaendelea.....



[1] Baqara/ 27.

[2] Ra’d/ 25.

[3] Muhammad (s.a.w.w)/ 22 – 23.

[4] Al- kaafiy, 2/346/ hadith 1.

[5] Al- kaafiy, 2/346/ hadith 2.

[6] Al- kaafiy, 2/346/ hadith 8.

[7] Al- kaafiy, 2/346/ hadith 5.

[8] Al- kaafiy, 2/346/ hadith 4.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: