bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      12:05:31
News ID: 328

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


UMAUTI WAWAKARIBIA:

Amesema Imam Ali (a.s) katika hotuba yake:

"Ninajiepusha kwa Mwenyezi Mungu kutokana na madhambi yaharakishao nakama. Akauliza mmoja wao, je! Yapo madhambi yakaribishayo kifo haraka, akasema (a.s): Ndio, kuvunja undugu ni katika madhambi yakaribishayo umauti haraka.[1]

Na uhakika ni kwamba wakusanyikapo wanafamilia na kuliwazana wao kwa wao, hakika Mwenyezi Mungu huwazidishia riziki wanafamilia hao, ama familia ambayo hukusanyika na ilihali ni wenye kughadhibikiana, hakika Mwenyezi Mungu huwaondolea riziki na kuwapunguzia umri wa maisha yao, hata wakiwani katika wamchao Mungu.

WATAKUFA WOTE:

Mmoja katika wafuasi wa Imam Sadiq (a.s) alimshitakia uonevu na dhulma ya mmoja wa wana wa ami yake kwa kusema: ndugu zangu na wana wa ami zangu wananigandamiza mimi mno, kiasi kwamba wamechukua hisa yangu ya nyumba na hawakuniachia ila chumba kimoja, na endapo nitawashita mahakamani, ninaweza kuchukua walicho nacho.

Imam akasema: vuta subira atakupa faraja Mwenyezi Mungu karibuni. Alikubaliana na Imam na akarejea, mnamo mwaka 131 hijria, ulizuka ugonjwa na wote walifariki na hakubaki hata mmoja, kisha akamjia Imam Saidq (a.s), Imam alimuuliza: Vipi hali ya jamaa zako? Alijibu kuwa: Wallah wote walifariki, Imam akasema: Kuangamia kwao ni kwa sababu ya kutokiri makosa yao juu yako na kuvunja kwao undugu dhidi yako.[2]

HUONDOKA KWA REHEMA ZA MWENYEZI MUNGU:

Imepokelewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kuwa amesema: "Idhihirikapo elimu na ikaporomoka amali na zikateleza ndimi na zikakhitalifiana nyoyo za waja wa Mungu na wakavunja undugu, wakati huo atawalaani Mwenyezi Mungu na atawaziba masikio yao na kuwapogoa macho yao”.

Na amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Hapana dhambi ambayo Mwenyezi Mungu anastahiki kutoa adhabu kali kwa Mwenyewe duniani na kuandaa adhabu hiyo siku ya akhera kuliko dhambi ya uonevu na kuvunja undugu”.

Amesema tena (s.a.w.w): "Hatoingia peponi avunjaye undugu”.

Kutka kwa Jaabir kutoka kwa Abuu Jaafar (a.s) kuwa amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Ameniambia Malaika Jibril (a.s) ya kwamba harufu ya pepo hupatikana katika kwa muda miaka elfu moja, ambapo hawatoipata mdharau wazazi wake, na mvunjaji undugu, na mkongwe mzinifu – na vile vile harufu yake hupatikana katika njia ya mwendo wa miaka lfu mbili, ambapo hatoipata harufu hiyo mdharau wazazi wake na mvunjaji undugu”.

Amesema tena (s.a.w.w): "Kuvunja undugu huzuia dua kupokelewa”.

Na katika fadhila za Laylat al- Qadr imepokelewa kutoka kwake (s.a.w.w) kuwa amesema: "Anawasamehe Mwenyezi Mungu katika usiku huo wengi isipokuwa makundi manne: Mlevi wa pombe, mdharau wazazi wake, mvunjaji undugu na adui wa waumini”.

Itaendelea…..



[1] Al- kaafiy, 2/346/ hadith 7.

[2] Al- kaafiy, 2/346/ hadith 3.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: