bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      12:11:48
News ID: 330

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


HAPANA UJAMAA KWA TAJIRI NA FUKARA:

Imezoeleka kwa wanajamii kujikurubisha zaidi kwa jamaa zao wa karibu wenye uwezo na kutojali mafukara miongoni mwao, hata kama ikiwa ni undugu wa karibu mno, lakini hapana katika sheria tafauti katika hukumu ibaguayo undugu na kuuvunja kati ya jamaa wa karibu. Ndio kila uwapo ukaribu wa karibu mno na yakapungua mawasiliano baina yao ndivyo hukumu inavyozidi katika hukumu yake.

KUFANYA KIBRI KWA NDUGU FUKARA NI SAWA NA HUKUMU YA KUVUNJA UNDUGU:

Katika vigawanyo vibaya vya uvunjaji undugu ni mtu kutomjali nduguye kwa ufukara wake, kutokana na mali pamoja na utajiri anaomiliki na umashuhuri wa kidunia, kwani mfano wake ni wale wasiojali undugu wa maskini na kujikurubisha kwa tajiri huyo humtendea kiburi, laiti kama atakuwa ni tajiri mwenzie humpa heshima na kumkaribisha, hakika kitendo hiki hakihesabiki kuwa ni kuunga undugu bali huwa ni kujali hali ya mazingira ya kidunia si kwa mtu yule nduguye wa karibu kwa sababu ya umasikini wake.

KUMTENDEA HISANI MOSAJI:

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Usimsaliti aliyekusaliti ukawa mithili yake na usivunje undugu na aliyekata undugu nawe”.[1]

Amesema tena (s.a.w.w): "Je! Nikuongozeni kwenye amali njema ya dunia na akhera? Wakasema: ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu: akasema (s.a.w.w): Ni yule mwenye kuunga undugu na aliyeukata na akampa aliyemnyima na akamsamehe aliyemdhulumu”.

HAKUPINGANI KUKATA UNDUGU PAMOJA NA KUMCHUKIA KAFIRI:

Katika yale yaliyotajwa juu ya kuunga undugu na uharamu wa kuukata na kutokuwepo tafauti kati ya kafiri na Mwislamu, na kati ya mwema au mwovu, basi haipingani maudhui haya pamoja na uharamu wa kusuhubiana na kafiri, mwovu na wajibu wa kuwachukia, kwa sababu kuunga undugu ni njia njema na kuamiliana pamoja na ndugu kwa kiasi ambacho itafahamika kuwa si undugu wa karibu mno, na haipingani na kufuata mwenendo mwema huu pamoja na kumchukia na kupingana naye kwani jambo hili ni jambo la kiroho na dhati.

ENDAPO HATOMUUNGA MKONO KAFIRI:

Ndio, ikiwa kuunga undugu huo itapelekea ujasiri na uthubutu wa kuzidisha ukafiri wake na uovu wake, kiasi kwamba ikiwa atakata undugu huo ataweza kuacha ukafiri na uovu wake, hapana pingamizi katika hilo katika mlango wa kukemea mabaya, na pamoja na kupata matumaini ya kwamba kukata undugu huo ni sababu ya kuacha kwake mambo hayo inawajibika kufanya hivyo, ama katika mahala pengine kuhusu nafasi za yakini na uwezekano wa kuacha ukafiri na uovu itabaki uharamu wa kuvunja undugu katika hali yake.

YAPASWA KUMFUKUZA ADUI WA DINI:

Na hapa ni mahali pengine kwa wajibu wa kukata undugu na kafiri na mwovu na hapo ni pale ambapo kwamba itakuwa ni katika hatua ya uadui na vita kwa ajili ya dini, kama asemavyo Mwenyezi Mungu mtukufu katika surat al- Mujaadala:

"لَا تَجِدُ قَوْمًا يؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيوْمِ الْآخِرِ يوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ".

"Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao”.[2]

IKIWA HAKUCHUPA MIPAKA NI WAJIBU KUUNGA UNDUGU:

Na anasema Mwenyezi Mungu mtukufu katika surat al- Mumtahina:

" لَا ينْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيهِمْ إِنَّ اللَّهَ يحِبُّ الْمُقْسِطِينَ . إِنَّمَا ينْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ".

"Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhalimu”.[3]

UDHAIFU KATIKA WAVUNJAO UNDUGU:

Hapana shaka ya kwamba kwa mujibu wa mitazamo ya Waislam na Riwaya za kimadhehebu yao ni kwamba kuunga undugu ni jambo la wajibu katika jamii, na kuuvunja ni haramu, pia ni miongoni mwa madhambi makubwa.

Ukafiri pamoja na ufasiki ni dalili zinazopelekea kuvunja undugu. Kwani siku moja Ibn Hamid alimuuliza Imamu Swadiq(a.s) kuwa:

Hakika ndugu zangu si miongoni mwa wale wanaofuata dini yangu. Je! Ndugu hao wanahaki za kimsingi kutoka kwangu? Akasema Imamu (a.s): Ndio, kwani haki ya undugu ina kipao mbele kuliko kitu chochote kile na wala haipotei kwa sababu ya jambo fulani. Lakini iwapo ndugu zako watakuwa ni miongoni mwa wanaofuata dini yako, basi wana haki aina mbili juu yako: Haki ya undugu pamoja na haki ya Uislam.

Imamu amesema: "Ikiwa utaunga undugu naye ila yeye akauvunja, basi Mwenyezi Mungu ataupa nguvu na kuwaunganisha, na iwapo utauvunja, naye akauvunja basi Mwenyezi anawadhoofisha nyote wawili”.

----------------------



[1] Al- Kaafiy: juz 2, uk 156, mlango wa Silat al- Rahim, hadith 24.

[2] Al- mujaadala/ 22.

[3] Al- Mumtahina/ 8 – 9.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: