bayyinaat

Published time: 17 ,November ,2018      18:08:57
Japokuwa Wakristo wanaoshikamana na dini wana imani ya mwokozi aliyeahidiwa, lakini uliberali ambao ndiyo mfumo wa kifikra unaotawala huko ....
News ID: 365

Wamagharibi wanasemaje?

Japokuwa Wakristo wanaoshikamana na dini wana imani ya mwokozi aliyeahidiwa, lakini uliberali ambao ndiyo mfumo wa kifikra unaotawala huko Magharibi haukubali itikadi hiyo. Kwa msingi huo maliberali wanasema, itikadi ya kudhihiri mwokozi aliyeahidiwa na ushindi wa haki dhidi ya batili katika kipindi cha akher zamaan ni njozi zisizo na ukweli. Hii ni licha ya kwamba, Mitume wote wa Mwenyezi Mungu walisisitiza fikra hii ya ushindi wa haki dhidi ya batili na kudhihiri mwokozi katika aheri zamani. Itikadi hii pia imesisitizwa na wanafalsafa wengi kwa kutumia hoja za kimantiki.

Wakati huo huo, sifa ya kutoa matumaini mema ya itikadi hii ya kudhihiri kwa mwokozi aliyeahidiwa katika mwisho wa zama na taathira zake nzuri kwa mtu binafsi na jamii imezidisha wimbi la watu kuamini itikadi hiyo duniani. Hii leo sambamba na kukithiri dhulma, ufisadi, ubaguzina uonevukatika maeneo mbalimbali ya dunia, fikra na itikadi ya kudhihiri mwokozi aliyeahidiwa pia inaenea na kupanuka zaidi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, itikadi hii inawapa watu matumaini ya kukomeshwa dhulma na uonevu na kuwahamasisha zaidi kupambana na mafisadi na madhalimu. Kwa msingi huo kwa kuwa mfumo wa ubepari hauwezi kukana mwenendo huu wa kuwepo kasi kubwa ya kuelekea kwenye itikadi ya mwokozi wa aheri zamani, baadhi ya wanadharia wa kimagharibi wamejitahidi kubuni fikra potofuya "mjitimilifu" au Utopia. Kwa kutumia mbinu mbalimbali na nyenzo kama tasnia ya filamu, Wamagharibi wanafanya njama za kupotosha itikadi ya mwokozi wa ulimwengu na kuiarifisha Marekani kuwa ndiyo jamii timilifu na ya uokovu wa mwanadamu.

Kwa hakika jitihada hizi za kutaka kuiarifisha jamii ya Marekani kuwa ndiyo jamii kigezo, timilifu na ruwaza njema ni kichekesho na penginekioja na maskhara. Hii ni kwa sababu, viongozi wa jamii hiyo ni wawakilishi wa mfumo wa ubepari ambao wako tayari kufanya jinai na uhalifu wa aina yoyote duniani kwa ajili ya kulinda na kubakisha hai mfumo huo. Si hayo tu, bali hata katika jamii hiyo hiyo ya Marekani kuna watu wengi wanaoamini kuwa, Issa Masia atarejea na kufanya mageuzi na marekebisho katika jamii hiyo na ulimwenguni kote.

Tishio dhidi ya itikadi ya kudhihiri Imam Mahdi AF

Katika mazingira ya sasa ya dunia, fikra na itikadi ya kudhihiri mwokozi aliyeahidiwa inakabiliwa na vitisho kutoka pande mbili. Kwa upande mmoja mabepari wenye nguvu na makundi ya madhalimu duniani ambayo yanakutambua kudhihiri kwa mwokozi aliyeahidiwa kwa ajili ya kueneza uadilifu na usawa na kupambana na dhulma na uonevu kuwa ni pigo na tishiokwa maslahi yao haramu, wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba, wanazuia kuenea zaidi itikadi hiyo inayozidisha matumaini ya mustakabali mwema wa wanadamu wote au kwa uchache wanafanya njama za kupotosha itikadi hiyo. Katika upande wa pili itikadi na fikra ya mwokozi wa ulimwengu kama zilivyo itikadi nyingine takatifu, haikusalimika na upotoshaji na hurafa kama tunavyoona tafsiri zisizo sahihi zinazotolewa kuhusiana na fikra ya kuwepo Imam Mahdi na jinsi ya kumsubiri mwokozi huyo. Kwa mfano tu, huko Marekani kuna baadhi ya watu wanaosubiri kudhihiri tena kwa Nabii Issa Masia wanaosema, kwa kuwa katika kipindi cha zama za mwisho wa duniaufisadi na ufuska vitakithiri sana, hivyo kuna ulazima wa kutayarisha uwanja na mazingira ya kudhihiri Yesu Kristo kwa kueneza uifisadi,ufuska na maovu! Tafsiri kama hizo zinaonekana pia kati yabaadhi ya Wakristo na hata miongoni yabaadhi ya Waislamu.

Hivyo basi kuna ulazima wa kurejea katika mafundisho ya Qur'ani na Hadithi sahihi ili kuzuia upotoshaji wa fikra ya mwokozi,kudhihiri na jinsi ya kumsubiri Imam Mahdi (as).

Itaendelea…….


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: