bayyinaat

Published time: 18 ,November ,2018      12:12:48
News ID: 369

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amekutana na kufanya mazungumzo mjini Tehran na Rais Barham Ahmed Salih wa Iraq na kusema kuwa, njia ya kuvuka matatizo na kukabiliana na njama za wasiotaka mema ni kulinda umoja wa kitaifa wa Iraq, kuwafahamu vizuri marafiki na maadui na kusimama imara mbele ya adui sanjari na kuwategemea vijana na kulinda na kuimarisha mahusiano na umarjaiya au wanazuoni wa kidini.

Ayatullah Khamenei amebainisha furaha yake kutokana na kufanyika kwa mafanikio makubwa uchaguzi wa bunge nchini Iraq na kisha kuchaguliwa Rais na Waziri Mkuu pamoja na maafisa wengine wa nchi hiyo na hivyo kuleta utulivunchini humo. Ameendelea kusema kuwa,baada ya duru za udikteta, hivi sasa Wairaqi wanamiliki nchi yao na wana uhuruwa kuchagua viongozi wao. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, baadhi ya serikali na nchi zisizoitakia mema Iraqzinataka Wairaqi wasionje ladha ya ushindi na mafanikio yao makubwa na wanachotaka wao ni kukosekana utulivu katika nchi hiyo na katika eneo hili lote la Mashariki ya Kati.

Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa, njia pekee ya kukabiliana na njama hizi ni kuhifadhi na kuimarisha umoja miongoni mwa makundi ya Wairaqi, wawe Waarabu auWakurdi au Mashia au Masuni.

Kadhalika amesema kuwa, kumfahamu kwa njia sahihi rafiki na adui ni muhimu sana katika sera za kigeni na kuongeza kuwa, baadhi ya serikali za eneo hili na nje ya eneo zina chuki kubwa sana dhidi ya Uislamu, Ushia, Usunni na nchi ya Iraq, hivyo zinaingilia masuala ya ndani ya Iraq. Amesema, kuna haja ya kusimama kidete na kwa uwazi kupambana na adui muovu.

Ayatullah al-Udhma Khamenei amesema, viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wana azma imara ya kuimarisha uhusiano na Iraq na kuongeza kuwa, yeye binafsi ana imani na suala hilo. Amesema: "Iraq azizi, yenye nguvu, yenye mamlaka na iliyostawi ni yenye faida kubwa kwa Iran na sisi tutabaki pamoja na ndugu zetuWairaqi."

Sayyid Ali Khamenei aidha ameashiria kushiriki wafanya ziara Wairani wapatao milioni mbili katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS mwaka huu na kusema kuwa, nyoyo za Wairani waliorejea nyumbani kutoka kwenye matembezi hayo zilijaa shukrani kutokana na ukarimu wa watu wa Iraq.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: