bayyinaat

Published time: 21 ,November ,2018      18:47:03
News ID: 372


Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Brazil imezindua kampeni yenye anuani ya "Muhammad SAW, Mtume wa Walimwengu" kwa lengo la kumtambulisha Mtume Mtukufu wa Uislamu.

Jumuiya hiyo imesema kuwa, inazindua kampeni hiyo ambayo imependekezwa na Wizara ya Wakfu ya Misri. Kama sehemu ya kampeni hiyo, Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Brazil imesema itasambaza vitabu la lugha ya Kireno kuhusu Sira ya Mtume Muhammad SAW. Aidha jumuiya hiyo imepanga kuandaa sherehe za Maulid ya Mtume SAW katika misikiti iliyo chini yake.

Kampeni ya "Muhammad SAW, Mtume wa Walimwengu" ni kampeni ya kimataifa ambayo imeanzishwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Misri kwa lengo la kumtambulisha Mtume Muhammad SAW kwa Walimwengu wote.

Kampeni hiyo ni kwa mujibu wa Aya ya 107 ya Suratul Anbiya katika Qur'ani Tukufu isemayo kuwa: "Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote."

Kampeni hiyo inakwenda sambamba na siku hizi za maadhimisho ya maulidi na kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW ambapo maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu yanashuhudia maadhimisho hayo ya uzawa wa mbora wa viumbe.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: