bayyinaat

Published time: 15 ,September ,2021      00:18:09
TARJUMA YA KITABU CHA (KIPIA KUMHUSU HUSEIN) - 001
hakika wingi wa vitabu na tungo juu ya historia ya Imam Husein na harakati yake (as) hautoshi, bali bado haja ipo ya kupatikana kitu kipya kwa sababu maudhui na mada yake ni pana zaidi ya yote yaliyoandikwa. Halikadhalika wingi wa tafiti zilizofanya haujatolesheleza mahitaji yaliyopo. Haja bado ipo ya kufanya utafiti wa kina zaidi ili kufichua ubora wa cheo chake na undani wa historia ya harakati yake(as).
News ID: 435

Bismillahi Ar-Rahmani Ar-Rahim

Shukran zote ni za mwenyezi Mungu (swt) Mola na Mlezi wa walimwengu wote kisha swala bora na salamu ziwe juu ya bwana na Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w) na Aali zake watoharifu.

Ama baada ya haya, hakika wingi wa vitabu na tungo juu ya historia ya Imam Husein na harakati yake (as) hautoshi, bali bado haja ipo ya kupatikana kitu kipya kwa sababu maudhui na mada yake ni pana zaidi ya yote yaliyoandikwa. Halikadhalika wingi wa tafiti zilizofanya haujatolesheleza mahitaji yaliyopo. Haja bado ipo ya kufanya utafiti wa kina zaidi ili kufichua ubora wa cheo chake na undani wa historia ya harakati yake(as).

Hii ni kwa sababu Husein ni mradi wa kimungu tangu Mwenyezi Mungu alipoumba. Asili yake imetokana na mchanganyiko wa Ardhi na utume wa babu yake, Nabii (s.a.w.w), na wito wake utaendelea katika vizazi vyote mpaka Mwenyezi mungu (swt)atakapomtuma Al-Mahdi (as) kulipiza kisasi chake, na kukomesha udhalimu uliopo katika uso wa Ardhi na kujaza usawa na uadilifu.

Nimependelea kuandika Mada zipatikanazo katika historia na misimamo yake (as) ambayo ndani yake kutakuwa na Jipya lenye kufaidisha watu wote hasa kwa Mahatibu wa Mimbari ya Husein (as).

Utapata kuona kuwa nimetegemea sana Hadithi zipatikanazo katika (kitabu cha) Kamil Az-Ziarat cha Faqihi mkubwa Ja'far bin Muhammad bin Qulawayh ambaye ni mwalimu wa Sheikh Mufid(ra) na sababu ya hili ni umakinifu wa kitabu chake Kamil Az-ziarat, ustadi na utoshelezaji wake. Kivyangu ninauona usahihi wa yote aliyoyapokea katika kitabu hiki.

Ninamuomba Allah (swt) atujumuishe katika rehema yake na rehema iliyo bora zaidi ni uombezi wa Husein (as).

Ali al-Kourani al-Ameli

Qom al-musharaf, Rajab al-Mukarram 1441 hjr- April 2020 AD.

MADA YA KWANZA

TURBA YA KARBALA NA TASBIHI YA KARBALA

Harufu ya Mchanga wa Karbala

Rafiki yangu aliniambia huku uso wake ukiwa na furaha: Nitakuzawadia zawadi uipendayo. Basi akatoa kutoka kwenye mfuko wake Tasbih ya Udongo. Mara macho yangu yakagubikwa na machozi. Nikaipokea kwa mikono yangu miwili na kuinusa. Nikayafuta macho yangu kwa shanga zake kisha nikamwambia:

"Ahsante mara mia...hakika hii ni ya Karbala kweli. Ni harufu asili ya mchanga wa Husein(as).

Ninakushukuru kwa kuwa hujaweka marashi ndani yake na kumfanya mtu kama mimi kupata ugumu wa kuitofautisha."

Akasema: Je, unatofautisha mchanga wa Karbala kwa harufu?

Nikasema: Ndio, ikiwa mpya na wala haijachanganywa na harufu nyingine.

Akasema: Je, unaweza kunisifia harufu yake?

Nikasema: una mvuto wa kipekee, na marashi ambayo si katika marashi ya duniani, kuna maana nyingi zisizoonekana ambazo utazifahamu kwa harufu na inakuwa vigumu kuzielezea.

Akasema: Hakika harufu ni Elimu!

Nikasema: Kunusa ni ulimwengu kabla haijakuwa Elimu... inamfugukia mwanadamu kwa mapenzi na anafahamu harufu za mpenzi wake kwa kulingana na kiwango cha imani yake, na anajuwa harufu za wazuri na wabaya.

Je! hujasoma kuwa Malaika wanajua Nia chema na mbaya ya Mwanadamu kutokana na harufu yake!

Ewe rafiki... lau kama wasomi wakubwa wa Hisia na kunusa wangekuwa pamoja na Yakub (as) hawangelihisi harufu ya Yusuf (as), ikiwa alikuwa hana Mapenzi na Imani.

Je! uliwahisikia riwaya ambayo inasema kuwa Ibrahim (as) alipitia Karbala akaunusa mchanga wake kisha akaswali ndani yake, na akainunua ardhi yake kutoka kwa wamiliki wake kisha akiita (Karblaa)!

Na je! ushawahi sikia kuwa Kamusi ya lugha ya Waashuri iliyokusanywa na masomi wa Kimagharibi inataja kuwa maana ya (كربو - لو ( : dhabihu ya Mtu, na maana ya (كربو - ئيل ( : dhabihu ya Mungu, na pia (كركميش ( : ina maana hii hii, basi staajabu utakavyo staajabu!

Je ushawahisikia kuhusu udongo alioletewa Mtume (saw) na Jibril au Mikail (as) kutoka Ardhi ya Karbala na kumwambia kuwa hakika huu ni udongo wa Ardhi ambayo Umma wake utamuuwa mtoto wake Hussein (as)! Kwahiyo akauweka kwa Umu Salama ukiwa ndani ya chupa , na kisha akamwambia (Ummu Salama) : Ikiwa ni siku ya Ashura na akauliwa Hussein (as) , udongo kwenye chupa utabadilika kuwa damu halisi, yaani safi!

Na je ushawahisikia kuwa Ali (as) alipitia Karbala, na akaubusu mchanga wake kisha atoa habari kwa yatakayotokea katika Ardhi hii!

Hakika hawa watukufu hufahamu mambo na matukio mengi kupitia kunusa kulingana na daraja yao.

Na hii ndio Elimu ya kunusa baada ya ulimwengu wa kunusa, ewe rafiki yangu!

Rafiki yangu akasema: Na je kunaye leo ambaye anafahamu uzuri na ubaya kutokana na harufu yake?

Nikamwambia : kama utataka maarifa ya uhakika kabisa, basi utayapata kwa Imam Mahdi (as), lakini ukitaka maarifa ambayo huenda yakapatia au yakaenda kinyume na hali halisi, basi utapata kwa Mu’mini kulingana na daraja ya Imani yake, usafi na utulivu wa roho yake… Ama huoni kuwa kunawakati mwingine unanusa harufu ya watu ambao Roho zao ni mbaya na nia zao ni chafu, hauwezi kustahamili kuondea wala kukaa nao!

Na unasikia kutoka kwa mtu harufu ya nia nzuri, kanakwamba upepo umepepea kutoka mbinguni!

Rafiki yangu akasema: Je! kuhusu kugeuka mchanga uliokuwa kwa Ummu Salamah kuwa damu wakati Hussein (as) alipouawa?

Nikamwambia : Hii hadithi ni Mutawatir katika maana, imepokewa Zaidi katika vyanzo vya Masuni, kama vile Musnad Ahmad (6/294), muulize utakaye kuhusu tafsiri yake , bila shaka atainamisha kichwa na kusema sijui!

HADITHI AMBAYO BADO INANISHANGAZA!

Lakini kabla ya kuanza mazungumzo katika hili, nakusimulia hadithi ambayo ilinishangaza na bado ipo kwenye akili yangu… Inasema: Hussein (as) aliugua na ugonjwa wake ukazidi zaidi, kwahiyo Fatimah (as) akampeleka kwa Mtume (saw) akimlilia na kumuomba msaada, akasema: Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu , muombe Allah amponeshe mtoto wako, na akamkabidhi mikononi mwake, Mtume (saw) akasimama na kukaa mbele ya kichwa chake, kisha akasema: Ewe Fatimah ewe mtoto wangu, hakika Mwenyezi Mungu aliyekuzawadia huyu ndiye mwenye uwezo wa kumponesha. Jibril akashuka na kumwambia Mtume : Ewe Muhammad, hakika Mwenyezi Mungu hajakuteremshia Sura katika Qur’ani ila ndani yake kuna " " فاء, na wala haiwi " الفاء” ila katika majanga tu ispokuwa Suratul-Hamdi, haina " فاء” , itisha kikombe chenye maji na ukisomee Al-Hamdu mara 40 kusha umumwagie , hakika Mwenyezi Mungu atamponya, akafanya hivyo, papo hapo akapona.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: