bayyinaat

Published time: 08 ,February ,2022      07:19:31
ULIZA UJIBIWE 003
Ni nini msimamo wa mashia kuhusu Ahlal Sunnah wal Jamaa bila kuzingatia Takia.
News ID: 438
00003-
Swali:
Ni nini msimamo wa mashia kuhusu Ahlal Sunnah wal Jamaa bila kuzingatia Takia.

Jawabu:
Ahlul sunna Wal jamaa ni ndugu zetu waislamu, tunaowana nao, tunakula chakula Chao, ni haramu kumwaga damu yao, na wao ni tohara, wanawapenda Ahlul Bait.
Madhehebu yote yanakubaliana mwenye kutamka shahada mbili anakuwa muislamu. 
Na mtu anaposilimu tu, mambo hayo yanathibiti.
Naam mwenye kuwachukia Ahlul Bait masuni na mashia wanamuita kuwa nasibi, na anakasoro Katika imani yake kwani kuwapenda Ahlul Bait kumetajwa wazi ndani ya Quran.
قُلْ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَی
(suratu Shura /23)
(Sema: siwaombi malipo yoyote ya (huu ujumbe niliowafikishia) ila tu kuwapenda watu wangu wa karibu (Ahlul Bait). 

Hawa manawasibu hatuoani nao kwani watawalea watoto wetu kuwachukia Ahlul Bait, na mwishowe kukosa radhi ya Allah.
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: