bayyinaat

Published time: 08 ,February ,2022      07:22:44
INNA LILLAHI WA INNA ILEIHI RAJI'UN.
AYATULLAH AL-UDHMA LUTFULLAH SWAFI GULPEIGANI. Tumempoteza tena mwanachuoni mwingine. Taa iliyong'aa kwa muda wa miaka 102, imerudi kwa Mola wake leo hii katika mji mtukufu wa Qum
News ID: 439
INNA LILLAHI WA INNA ILEIHI RAJI'UN.
AYATULLAH AL-UDHMA LUTFULLAH SWAFI GULPEIGANI.
Tumempoteza tena mwanachuoni mwingine. Taa iliyong'aa kwa muda wa miaka 102, imerudi kwa Mola wake leo hii katika mji mtukufu wa Qum, ambaye ni Ayatullah al-Udhma Sheikh Swafi Gulpaigani. Alikuwa na dauru kubwa katika kuasisi mfumo unaoiendesha jamhuri ya kiislamu ya Iran. Alikuwa kiungo muhimu katika jopo la wanachuoni walio andaa katika mijadala mirefu katiba ya nchi ya kiislamu. Aliteuliwa na Imam Khomeini kuwa kiongozi wa kwanza wa Bunge la Wataalamu wa Katiba kwa miaka minane. 
Katika miaka 30 aliyoishi akiwa marjii taqlid, baada ya kuichukuwa nafasi ya mkwe wake, marehemu Ayatullah al-Udhma Sayyid Muhammad Ridha Gulpaigani, aliweza kuwalea wanafunzi wengi sana. Aliweza kufikia daraja ya marajii wakuu wa zama hizi.
Ameandika vitabu vingi na vya msingi, alikuwa mtetezi wa aqida ya Imam Mahdi (a.j.) na ana kitabu chake maarufu (muntakhabul athar) kuhusiana na Imam (a.j.). Alikuwa mwepesi wa machozi katika misiba ya Ahlul bait (a.s.) bali alikuwa na ada ya kuweka masira ya kumuomboleza Bibi Fatima (a.s.) kila mwaka.
Tunampa rambirambi Swahibuz Zaman (a.j) marajii taqlid wote, waumini, Haoza ya Qum, familia yake na wakazi wa mji alipozaliwa, mji wa Gulpaigan.Allah amuunganishe na Mtume (s.a.w.a) na Ahlul bait (a.s.).

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: