bayyinaat

Published time: 26 ,May ,2017      18:17:21
“Enyi watu! Hakika milango ya pepo katika mwezi huu huwa wazi, basi muombeni mola wenu asiwafungie, na pia milango ya moto katika kipindi hiki huwa imefungwa..........
News ID: 90


Mwendelezo wa hotuba ya Mtume....

وَ مَنْ تَطَوَّعَ فِیهِ بِصَلَاةٍ کتَبَ اللَّهُ لَهُ بَرَاءَةً مِنَ النَّارِ وَ مَنْ أَدَّی فِیهِ فَرْضاً کانَ لَهُ ثَوَابُ مَنْ أَدَّی سَبْعِینَ فَرِیضَةً فِیمَا سِوَاهُ مِنَ الشُّهُورِ

" Na mwenye kuswali swala ya sunna katika mwezi huu basi huandikwa katika walioepushwa na moto, na mwenye kufanya jambo lolote la faradhi basi hupata malipo ya aliyefanya faradhi sabini katika miezi mingine...”

وَ مَنْ أَکثَرَ فِیهِ مِنَ الصَّلَاةِ عَلَی ثَقَّلَ اللَّهُ مِیزَانَهُ یوْمَ تَخِفُّ الْمَوَازِینُ

"Na mwenye kuniswalia sana mimi (Mtume) basi mizani yake itakuwa mizito siku ambayo kuna mizani itakuwa haina kitu...”

وَ مَنْ تَلَا فِیهِ آیةً مِنَ الْقُرْآنِ کانَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ خَتَمَ الْقُرْآنَ فِی غَیرِهِ مِنَ الشُّهُورِ

" Na mwenye kusoma aya moja tu katika Quran hupata malipo ya aliyehitimisha Quran yote katika miezi mingine...”

أَیهَا النَّاسُ إِنَّ أَبْوَابَ الْجِنَانِ فِی هَذَا الشَّهْرِ مُفَتَّحَةٌ فَاسْأَلُوا رَبَّکمْ أَنْ لایغَلِّقَهَا عَلَیکمْ وَ أَبْوَابَ النِّیرَانِ مُغَلَّقَةٌ فَاسْأَلُوا رَبَّکمْ أَنْ لایفَتِّحَهَا عَلَیکمْ

"Enyi watu! Hakika milango ya pepo katika mwezi huu huwa wazi, basi muombeni mola wenu asiwafungie, na pia milango ya moto katika kipindi hiki huwa imefungwa, basi muombeni mola wenu asiifungue...”

وَ الشَّیاطِینَ مَغْلُولَةٌ فَاسْأَلُوا رَبَّکمْ أَنْ لایسَلِّطَهَا عَلَیکمْ

"Na mashetani pia huwa wamefungwa, basi muombeni mola wenu asiwafungue...”

قَالَ أَمِیرُ الْمُؤْمِنِینَ(ع) فَقُمْتُ فَقُلْتُ یا رَسُولَ اللَّهِ مَا أَفْضَلُ الْأَعْمَالِ فِی هَذَا الشَّهْرِ

Imamu Ally as anasema "baada ya hapo nilisimama na kumuuliza Mtume, je, ni jambo gani bora sana katika mwezi huu?”

Kisha mtume saww akamjibu kwa kumwambia:

فَقَالَ یا أَبَا الْحَسَنِ أَفْضَلُ الْأَعْمَالِ فِی هَذَا الشَّهْرِ الْوَرَعُ عَنْ مَحَارِمِ اللَّهِ عَزَّ وَ جَلَّ

Ewe Abal Hassan, hakika jambo bora zaidi katika mwezi huu ni kujikinga na kila ambalo Mwenyezi Mungu ameliharamisha...”

Baada ya mtume kutoa jibu hilo alianza kulia, na alipoulizwa na Imamu Ally juu ya kilio chake hicho alisema:

َقَالَ یا عَلِی أَبْکی لِمَا یسْتَحَلُّ مِنْک فِی هَذَا الشَّهْرِ کأَنِّی بِک وَ أَنْتَ تُصَلِّی لِرَبِّک وَ قَدِ انْبَعَثَ أَشْقَی الْأَوَّلِینَ وَ الْآخِرِینَ شَقِیقُ عَاقِرِ نَاقَةِ ثَمُودَ فَضَرَبَک ضَرْبَةً عَلَی قَرْنِک فَخَضَبَ مِنْهَا لِحْیتَک

Ewe Ally, hakika nalia juu ya ambayo yatakuja kukukuta katika mwezi huu, kana kwamba nakuona upo katika hali ya kumsalia mola wako, na anakujia mwovu wa waovu, mfano wake ni yule aliyemchinja ngamia wa watu wa Thamud, ambapo anakupiga pigo moja katika kichwa chako na kusababisha damu kuenea katika ndevu zako...”

قَالَ أَمِیرُ الْمُؤْمِنِینَ(ع) فَقُلْتُ یا رَسُولَ اللَّهِ وَ ذَلِک فِی سَلَامَةٍ مِنْ دِینِی فَقَالَ فِی سَلَامَةٍ مِنْ دِینِک

Imamu Ally akamuuliza Mtume: "je, hali hiyo itanikuta huku nikiwa na usalama katika dini yangu?”. Mtume saww akajibu "naam utakuwa katika usalama wa dini yako”.

ثُمَّ قَالَ یا عَلِی مَنْ قَتَلَک فَقَدْ قَتَلَنِی وَ مَنْ أَبْغَضَک فَقَدْ أَبْغَضَنِی وَ مَنْ سَبَّک فَقَدْ سَبَّنِی لِأَنَّک مِنِّی کنَفْسِی رُوحُک مِنْ رُوحِی وَ طِینَتُک مِنْ طِینَتِی

"Kisha Mtume akasema: "ewe Ally, hakika mwenye kukuua wewe ni kama ameniua mimi, na mwenye kukuchukiza wewe ni sawa amenichukiza mimi, na mwenye kukutukana wewe ni sawa na amenitukana mimi, kwani wewe kwangu mimi ni sawa na mimi, roho yako na mwili wako vinatokana na roho na mwili wangu..”

إِنَّ اللَّهَ تَبَارَک وَ تَعَالَی خَلَقَنِی وَ إِیاک وَ اصْطَفَانِی وَ إِیاک وَ اخْتَارَنِی لِلنُّبُوَّةِ وَ اخْتَارَک لِلْإِمَامَةِ فَمَنْ أَنْکرَ إِمَامَتَک فَقَدْ أَنْکرَ نُبُوَّتِی

Hakika Mwenyezi Mungu ameniumba mimi na wewe na amenichagua mimi na wewe, amenichagua mimi kuwa Mtume wake na amekuchagua wewe kuwa Imamu na kiongozi, basi mwenye kupinga uimamu wako ni sawa na mwenye kupinga utume wangu...”

یا عَلِی أَنْتَ وَصِیی وَ أَبُو وُلْدِی وَ زَوْجُ ابْنَتِی وَ خَلِیفَتِی عَلَی أُمَّتِی فِی حَیاتِی وَ بَعْدَ مَوْتِی أَمْرُک أَمْرِی وَ نَهْیک نَهْیی

Ewe Ally, hakika wewe ni mrithi wangu, na baba wa kizazi changu, na mume wa binti yangu, na khalifa wangu katika umma wangu wakati wa uhai wangu na baada ya kifo changu, uamrishalo na kukataza wewe ndilo niamrishalo na kukataza mimi...”

أُقْسِمُ بِالَّذِی بَعَثَنِی بِالنُّبُوَّةِ وَ جَعَلَنِی خَیرَ الْبَرِیةِ إِنَّک لَحُجَّةُ اللَّهِ عَلَی خَلْقِهِ وَ أَمِینُهُ عَلَی سِرِّهِ وَ خَلِیفَتُهُ عَلَی عِبَادِه

Naapa kwa ambaye amenituma kuwa mtume na kunifanya mbora wa viumbe vyote, ya kwamba wewe ni hoja ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe, na pia ni mwenye kuaminiwa katika siri zake, na pia ni khalifa wake kwa waja wake...”

Na hapo ndiyo mwisho wa hotuba hii, lakini bila shaka kuna mambo mengi sana ambayo yanapaswa kuongelewa katika hotuba hii, na hapa ndio nachukua fursa hii uiache kuungana nami katika wakati ujao ili tuweze kuchambua baadhi ya mambo ambayo yatakuwa na faida kwetu katika kuuendea mwezi mtukufu wa Ramadhani na hata pindi tutakapokuwa ndani ya mwezi huo.

Mwenyezi Mungu atujaalie tuweze kufanya yenye kumridhisha.

Sh Abdul Razaq Rashid.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: