bayyinaat

Published time: 26 ,May ,2017      18:26:24
kuna taratibu ambazo Mwislamu anatakiwa kushikamana nazo ili tu aweze kuuingia, kuishi nao na hata kuumaliza hali ya kuwa amefikia lengo ambalo Mwenyezi Mungu amelitaka kwa waja wake pale alipowafaradhishia kufunga kwa kusema :
News ID: 91


Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu

Bila shaka ni jambo lenye kufahamika kwa Waislamu wote kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani ni katika ile miezi mitukufu, lakini pamoja na hayo pia bado kuna utukufu ambao unauhusu tu mwezi huu wa Ramadhani. Na katika kuuelekea mwezi huu kuna taratibu ambazo Mwislamu anatakiwa kushikamana nazo ili tu aweze kuuingia, kuishi nao na hata kuumaliza hali ya kuwa amefikia lengo ambalo Mwenyezi Mungu amelitaka kwa waja wake pale alipowafaradhishia kufunga kwa kusema :

"enyi mlio amini!, hakika funga imekuwa lazima kwenu kama ambavyo ilikuwa lazima kwa waliokuwa kabla yenu ili muweze kumcha Mungu...”

Lakini lengo hili si kwamba linaweza kufikiwa tu bila ya kuwa na maandalizi katika kuuelekea mwezi au funga kwa ujumla. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutakuwa ni wenye kuungana na wewe msomaji wetu katika kuhakikisha kwamba kila siku unakuwa ni mwenye kupata na kujua ni mambo gani ambayo yanapaswa kufanywa ili tu tuweze kuufunga mwezi huu kwa usalama na mwisho wa siku tufikie lengo ambalo Mola anataka tufikie.

Hivyo tutaanza na mambo ambayo yanapaswa kufanywa katika usiku wa kwanza kabisa ikiwa ni pamoja na adabu na taratibu zake.

Adabu za usiku wa kwanza

Wanazuoni wetu wanatuhusia kushikamana na adabu ambazo wamezitaja kabla ya kuanza jambo zima la kufunga mwezi huu mtukufu, na adabu hizo ni kama ifuatavyo:

· Kuutafuta mwezi

Kwa maana ya kwamba Mwislamu awe ni mwenye harakati ya kutaka kujua kwamba mwezi umeandama au la?, na jambo hili kuna baadhi ya maulama wamesema kwamba ni lazima kwa kila mmoja aweze kuutafuta mwezi.

· Dua baada ya kuuona

Kwa maana ya kwamba baada ya kuutafuta na kuuona usiwe ni mwenye kuuashiria kwa vidole, bali badala yake uelekee kibla na usome dua ifuatayo huku ukiuambia mwezi ule:

رَبّي وَرَبُّكَاللهُ رَبُّ الْعالَمينَ، اَللّـهُمَّ اَهِلَّهُ عَلَيْنا بِالاْمْنِ وَالاِيمانِ، وَالسَّلامَةِ وَالاِسْلامِ، وَالْمُسارَعَةِ اِلى ما تُحِبُّ وَتَرْضى، اَللّـهُمَّ بارِكْ لَنا في شَهْرِنا هذا، وَارْزُقْنا خَيْرَهُ وَعَوْنَهُ، وَاصْرِفْ عَنّا ضُرَّهُ وَشَرَّهُ وَبلاءَهُ وَفِتْنَتَهُ

"Mola wangu na mola wako ni Mwenyezi Mungu mola wa walimwengu wote, ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba mwezi huu utujie kwa amani na imani, usalama na kujisalimisha kwako, na kuelekea kwa haraka yale ambayo unayapenda na kuyaridhia. Ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika mwezi huu, na turuzuku heri zake na utuondolee madhara na shari na mabalaa na mitihani....”

Na dua nyinginezo ambazo zimefundishwa na mtukufu Mtume saww zinazohusiana na swala la kuuona mwezi. Cha muhimu ni kwamba Mwislamu awe katika hali fulani ya mafungamano na mola wake baada ya kujiwa na mwezi huu. Mfano wa dua hizo ni kama ifuatayo:

اَيُّهَا الْخَلْقُ الْمُطيعُ الدّائِبُ السَّريعُ، الْمُتَرَدِّدُ في مَنازِلِ التَّقْديرِ، الْمُتَصَرِّفُ في فَلَكِ التَّدْبيرِ، آمَنْتُ بِمَنْ نَوَّرَ بِكَ الظُّلَمَ، وَاَوْضَحَ بِكَ الْبُهَمَ، وجَعَلَكَ آيَةً مِنْ آياتِ مُلْكِهِ، وَعَلامَةً مِنْ عَلاماتِ سُلْطانِهِ، فَحَدَّ بِكَ الزَّمانَ، وامْتَهَنَكَ بِالْكَمالِ وَالنُّقْصانِ، وَالطُّلُوعِ والاُفُولِ، وَالاِنارَةِ والْكُسُوفِ، في كُلِّ ذلِكَ اَنْتَ لَهُ مُطيعٌ، وَاِلَى اِرادَتِهِ سَريعٌ، سُبْحانَهُ ما اَعْجَبَ ما دَبَّرَ مِنْ اَمْرِكَ، وَاَلْطَفَ ما صَنَعَ في شَأنِكَ، جَعَلَك مِفْتاحَ شَهْر حادِث لاَمْر حادِث، فَاَسأَلُاللهَ رَبِّي وَرَبَّكَ، وَخالِقي وَخالِقَكَ، وَمُقَدِّري وَمُقَدِّرَكَ، وَمُصَوِّري وَمُصَوِّرَكَ اَنْ يُصَلِّيَ عَلى مُحَمَّد وآلِ مُحَمَّد، وَاَنْ يَجْعَاَلك هِلالَ بَرَكة لا تَمْحَقُها الاَيامُ، وَطَهارَة لا تُدَنِّسُهَا الاثامُ، هِلالَ اَمْن مِنَ الافاتِ، وَسَلامَة مِنَ السَّيِّئاتِ، هِلالَ سَعْد لا نَحْسَ فيهِ يُمْن لا نَكَدَ مَعَهُ، وَيُسْر لا يُمازِجُهُ عُسْرٌ، وَخَيْر لا يَشُوبُهُ شَرٌّ، هِلالَ اَمْن وَايمان وَنِعْمَة وَاِحْسان وَسَلامَة وَاِسْلام، اَللّـهُمَّ صَلِّ عَلى مُحَمَّد وَآلِ مُحَمَّد، وَاجْعَلْنا مِنْ اَرْضى مَنْ طَلَعَ عَلَيْهِ، وَاَزْكى مَنْ نَظَرَ اِلَيْهِ، وَاَسْعَدَ مَنْ تَعَبَّدَ لَكَ فيهِ، وَوَفِّقْنَا اَللّـهُمَّ فيهِ لِلطّاعَةِ وَالتَّوْبَةِ، وَاعْصِمْنا فيهِ مِنَ الاثامِ وَالْحَوبَةِ، وَاَوْزِعْنا فيهِ شُكْرَ النِّعْمَةِ، واَلْبِسْنا فيهِ جُنَنَ الْعافِيَةِ، وَاَتْمِمْ عَلَيْنا بِاسْتِكْمالِ طاعَتِكَ فيهِ الْمِنَّةَ، اِنَّكَ اَنْتَ الْمَنّانُ الْحَميدُ، وَصَلَّىاللهُ عَلى مُحَمَّد وآلِهِ الطَيِّبينَ، وَاجْعَلْ لَنا فيهِ عَوناً مِنْكَ عَلى ما نَدَبْتَنا اِلَيْهِ مِنْ مُفْتَرَضِ طاعَتِكَ، وَتَقَبَّلْها اِنَّكَ الاَكْرَمُ مِنْ كُلِّ كَريم، وَالاَرْحَمُ مِنْ كُلِّ رَحيم، آمينَ آمينَ رَبَّ الْعالَمينَ.

Adabu nyinginezo

Baada ya kuangalia adabu zinazohusiana na swala zima la kuutafuta mwezi na kusoma dua mahususi baada yake, pia kuna adabu nyinginezo ambazo maulama wanatuambia kwamba pia zinaambatana na mwezi huu mtukufu. Nazo ni:

1. Kukutana kimwili

Maulama wanasema kwamba jambo la mke na mume kukutana kimwili usiku wa kwanza wa mwezi huu ni suna, tofauti ni miezi mingine ambapo ni makuruhu kukutana kimwili mwanzoni mwa mwezi

2. Kuoga

Ni sunna sana kuoga kwa nia ya josho la usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani. Na imepokelewa kwamba mwenye kuoga josho hili basi hatopatwa na ugonjwa wa muwasho mpaka Ramadhani ijayo. Yaani anakuwa na dhamana ya kutopata gonjwa la ngozi kwa mwaka mzima.

3. Ziara

Imesisitizwa sana kwa wenye uwezo kuweza kwenda kumzuru mjukuu wa mtume saww, Imamu Hussein as, na ambao hawana uwezo wa kwenda lilipo kaburi lake basi watosheke na kusoma ziara ya mbali na Mwenyezi Mungu atamlipa malipo mema.

4. swala

ni sunna kuswali swala ambayo imesisitizwa sana katika usiku huu, nayo ni swala ya rakaa mbili, ambayo katika kila rakaa anasoma surat Fatiha na surat Al an-am mara moja, kisha amuombe Mwenyezi Mungu amkinge na mabalaa na magonjwa.

5. Quran

Kwa maana ya kwamba isomwe sana katika usiku huu, na imepokelewa kutoka kwa Imamu Sadiq as kwamba kabla ya kusoma Quran aseme:

اَللّـهُمَّ اِنّي اَشْهَدُ اَنَّ هذا كِتابُكَ الْمُنْزَلُ مِنْ عِنْدِكَ عَلى رَسُولِكَ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِاللهِ صَلَّىاللهُ عَلَيْهِ وآلِهِ، وَكَلامُكَ النّاطِقُ عَلى لِسانِ نَبِيِّكَ، جَعَلْتَهُ هادِياً مِنْكَ اِلى خَلْقِكَ، وَحَبْلاً مُتَّصِلاً فيـما بَيْنَكَ وَبَيْنَ عِبادِكَ، اَللّـهُمَّ اِنّي نَشَرْتُ عَهْدَكَ وَكِتابَكَ، اَللّـهُمَّ فَاجْعَلْ نَظَري فيهِ عِبادَةً، وَقِراءَتي فيهِ فِكْراً، وَفِكْري فيهِ اعْتِباراً، وَاجْعَلْني مِمَّنْ اتَّعَظَ بِبَيانِ مَواعِظِكَ فيهِ، وَاجْتَنَبَ مَعاصيكَ، وَلا تَطْبَعْ عِنْدَ قِراءَتي عَلى سَمْعي، وَلا تَجْعَلْ عَلى بَصَري غِشاوَةً، وَلا تَجْعَلْ قِراءَتي قِراءَةً لا تَدَبُّرَ فيها، بَلِ اجْعَلْني اَتَدَبَّرُ آياتِهِ وَاَحْكامَهُ، آخِذاً بِشَرايِعِ دينِكَ، وَلا تَجْعَلْ نَظَري فيهِ غَفْلَةً، وَلا قِراءَتي هَذَراً، اِنَّكَ اَنْتَ الرَّؤوفُ الرَّحيمُ

Na baada ya kusoma aseme:

للّـهُمَّ اِنّي قَدْ قَرَأتُ ما قَضَيْتَ مِنْ كِتابِكَ الَّذي اَنْزَلْتَهُ عَلى نَبِيِّكَ الصّادِقِ صَلَّىاللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ، فَلَكَ الْحَمْدُ رَبَّنا، اَللّـهُمَّ اجْعَلْني مِمَّنْ يُحِلُّ حَلالَهُ، وَيُحَرِّمُ حَرامَهُ، وَيُؤْمِنُ بِمُحْكَمِهِ وَمُتَشابِهِه، وَاجْعَلْهُ لي اُنْساً في قَبْري، وَاُنْساً في حَشْري، وَاجْعَلْني مِمَّنْ تُرْقيهِ بِكُلِّ آيَة قَرَأها دَرَجَةً في اَعْلى عِلِّيّينَ، آمينَ رَبَّ الْعالَمينَ

hizi ni baadhi ya adabu ambazo kwa imani yangu kila Mwislamu anaweza kushikamana nazo kwa usiku huu wa kwanza ili tu tuweze kufikia lengo ambalo muumba wetu anataka tulifikie.

Ramadhani Mubarak kwa Waislamu wote duniani.

Sh Abdul Razaq Rashid

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: