bayyinaat

Published time: 08 ,February ,2017      10:55:53
Je! Katika Qur’an tukufu kuna dhulma yoyote dhidi ya mwanamke?
News ID: 11

Je! Yafaa kumpiga Mwanamke?

Swali:

Je! Katika Qur’an tukufu kuna dhulma yoyote dhidi ya  mwanamke? Maana tunaona  katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

(وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا).

"Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika utiifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu”. Anisaai; 34.

Wanawake wengi hustaajabu kwamba, Je! si ushahidi wa kuhalalisha kumpiga mwanamke? Hivyo kwa nini baadhi wanakanusha hilo? Ni nini maana ya vipigo hapa?  Je! Ni kipigo kikali au kipigo cha kuzuia? Je, inaruhusiwa kumpiga?

Jawabu:

Kamwe hakuna dhulma katika Qur’an sio kwa wanaume au kwa wanawake, wote wamepewa na Mwenyezi Mungu haki na wajibu na majukumu, na miongoni mwa haki za Mume kwa mkewe, ni Mke kumwezesha mumewe na kutimiza mahitaji yake ya kijinsia na kufurahia halali hiyo.

Iwapo mke hatoheshimu haki hii na kutomtii mumewe na kuasi kile anachokitaka kutoka kwake, pasi na udhuru wowote, basi uasi huu utafuatiwa na hukumu za kisheria zilizotajwa katika Aya tukufu hapo juu, miongoni mwa hukumu hizo ni kupiga na mfano wa mengine kama yalivyotajwa katika vitabu vya kifiqhi.

Hivyo basi, kanuni hairuhusu kupiga kwa ukali, bali kwa utaratibu maalum, nayo ni kwa sababu maalumu na bayana, ambayo ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa uwezeshaji wa kijinsia baada ya kuanguka awamu ya pili ya ushauri na kuhama kitandani, na wala hakuathirika kutekeleza haki zote za mumewe.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: