Swali:
Mwenyezi
Mungu anasema:
(مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ
وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ
أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ).
"Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke,
naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora
ya waliyo kuwa wakiyatenda”. Nahl; 97
Mungu, ameelekeza maamuzi yake kwa Waislamu,
wanaume na wanawake kwa usawa lakini nani ambae hupangilia majukumu kati ya
mwanamke na mwanamume? Dini au jamii? Ni mwanamume peke yake anapaswa kuhusika
na siasa? Ni ipi nafasi ya Uislamu juu ya haki za wanawake katika siasa, kama
vile haki ya kupiga kura na haki ya kugombea halmashauri za ubunge na ofisi za
umma? Na ni lipi jukumu la mwanamke katika masuala ya umma na taifa? Je!
Huingia uongozi wa mwanamke kuongoza wanaume katika nafasi hii?
Jawabu:
Aya tukufu inaonyesha kwamba wanaume na
wanawake watakapo simamia utendaji wa amali kwa kumuelekea Muumba, na vilevile
kazi inayotakiwa kwa mtu binafsi na maisha ya kijamii pia, na akasimamia majukumu
yake kwa upande wa jamii, basi ataishi maisha mema katika dunia hii na atalipwa
mema kwa yale aliyofanya.
Lakini ni upi wadhifa wa mwanamume? Na ni ipi
kazi ya mwanamke? Aya si katika nafasi ya kulibainisha hilo, na haitumiki
kwamba wadhifa binafsi wa Mwanaume au kijamii ni sawa na wadhifa wa Mwanamke,
bali si mantiki kulinganisha hilo. Kwani sheria, akili na desturi hupambanua
wadhifa wa kila mmoja (Mwanaume na Mwanamke) kulingana na uwezo wao na uwezo
wa mwili na akili, na kwa msingi wa majukumu yao na ufanisi katika jamii ya
Wanadamu, kama vile haki za Mwanaume na Mwanamke huwa tofauti kisheria na kuwa
mfuasi kama inavyotakiwa kikawaida wanaume na wanawake ni kwa misingi ya
majukumu ya kila mmoja.