bayyinaat

Published time: 15 ,October ,2017      18:49:02
Ndoa ni jiwe la kwanza la msingi la kujenga familia, na familia ni taasisi kuu ya jamii. Licha ya kuwa ndoa kwa mtazamo mmoja linahesabiwa kuwa jambo la ........
News ID: 115

Ndoa ni jiwe la kwanza la msingi la kujenga familia, na familia ni taasisi kuu ya jamii. Licha ya kuwa ndoa kwa mtazamo mmoja linahesabiwa kuwa jambo la mtu binafsi, lakini katika upande mwingine, ni nguzo imara na madhubuti ya jamii ya mwanadamu. Faida na madhara yanayopatikana katika jamii taathira yake inatokana na ndoa. Kwa maana kwamba, kuimarika kwa ndoa katika jamii ni kuweko jamii bora na yenye maelewano, huba na kutawala furaha na buraha. Aidha kupuuzwa suala la ndoa hupelekea jamii kumomonyoka kimaadili na madhara yake ni kupatikana mahusiano haramu; na baya zaidi ni kuzaliwa watoto nje ya ndoa ambao hukosa haki nyingi. Ni kwa muktadha huo, ndio maana tunapata kuwa suala la ndoa limehesabiwa na dini zote za mbinguni kuwa ni jambo tukufu na muhimu mno, na takribani dini zote hizo zina mafunzo na maelekezo maalumu kwa ajili ya suala la ndoa na kufunga pingu za maisha. Hata katika jamii zilizobakia nyuma kabisa na ambazo pengine za majangwani utaona katika historia kuwa, ndoa lilikuwa jambo lililoheshimiwa na kupewa umuhimu maalumu.

Dini zote za mbinguni zimehamasisha suala la ndoa

Dini zote za mbinguni zinalitazama suala la ndoa kwa jicho maalumu la utukufu. Hata hivyo kati ya dini zote hizo za mbinguni, hakuna dini ambayo imeweka sheria za kushajiisha ndoa, maalumu na tukufu kama dini Tukufu ya Kiislamu. Kwa hakika familia ni kituo na taasisi tukufu ambayo jiwe lake la msingi huwekwa kwa jinsia mbili yaani jinsia ya kike na ya kiume kuoana na kituo hicho hukamilika mara wanapozaliwa, watoto ambao huja na kuimarisha misingi na nguzo za familia hiyo. Wana nadharia wanaamini kuwa, familia ndio taasisi ya kwanza ya dharura kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya maisha, huba na kubakia jamii. Familia ni nguzo ya jamii na inahesabiwa kuwa ni msingi muhimu. Uislamu umeweka mipango na mikakati maalumu ya kuboresha familia.

ما بُنِيَ في الإسلامِ بناء احب الي الله و اعز من التزويجقال رسول الله (ص) :

kiasi kwamba, Bwana Mtume Muhammad (SAW) amesema:

"Hakuna jengo lililojengwa katika Uislamu ambalo ni tukufu zaidi na lenye kupendwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kuoana (ndoa)."

Utendaji wa familia katika jamii ni sawa kabisa na utendaji wa seli katika kiumbe hai, kwani kwa kadiri seli hizo zinavyokuwa salama zaidi na zenye nguvu, ndivyo ambavyo mwili wa kiumbe hai unavyokuwa salama na wenye nguvu zaidi. Ndoa baina ya mke na mume, ni mfungamano wa kimaumbile na mahaba baina ya wanandoa hao, mfungamano ambao ni wa lazima kwa shabaha ya kuendeleza kizazi cha mwanadamu. Hata hivyo mtazamo huu unahitajia miongozo na usimamizi, kwani kinyume na hivyo, utaleta madhara na uharibifu. Katika Uislamu kuna vigezo vilivyoainishwa kwa ajili ya kujenga familia. Kadiri nguzo zinazounda familia zitakavyotabikiana na kuoana na vigezo hivyo, basi ni kwa kiwango hichohicho ustahiki na ubora utakavyokuwa.

Itaendelea.....


LABEL:
non-publishable: 0
Under Review: 0
Published: 2
2639/01/05 - 21:28
|
Iran, Islamic Republic of
|
Anonymous
0
0
Makala nzuri sana
Administrator Shukrani sana na pia karibu sana na endelea kutembelea mtandao huu
2639/01/11 - 12:33
|
Iran, Islamic Republic of
|
Anonymous
0
0
Shukran. Allah akujazi
Administrator karibu sana na endelea kutembelea mtandao huu
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: