KUMJUA MWENYEZI MUNGU (SWT)
Kwa msingi huu basi tunafikia katika hatua
ya kutambua kwamba kumbe huyu mwanadamu kwanza ana muumba wake, pili ni kwamba
muumba wa huyu mwanadamu anataka na anapenda kuona mwanadamu amefikia katika
malengo matakatifu ambayo yatakuwa ni faida kwa huyuhuyu mwanadamu.
Lakini je, ni jambo ambalo lipo wazi kwa kila mmoja wetu kwamba kuna muumba na anasifika na sifa gani?, au kwamba kuna malengo ambayo huyu muumba anataka sisi tuyafikie?, la hasha! Maana kama ingalikuwa hivyo basi kusingekuwa na tofauti mbalimbali katika kumuelekea huyo muumba. Hivyo kutokana na hayo yote kunakuwa na umuhimu wa kila mwanadamu kwanza kuweza kumtambua muumba wake pamoja na sifa zake anazostahiki kusifiwa nazo, pia kuweza kutambua sifa ambazo hapaswi kusifiwa nazo, na hatimaye ndio ataweza kutambua kwamba muumba mwenye sifa kama hizi atakuwa na malengo gani ambayo anataka mimi niyafikie.
Ni ipi njia sahihi ya kumjua Mwenyezi
Mungu?, na je, kuna ulazima wa kumjua Mwenyezi Mungu?. Haya ni maswali mawili
ambayo yatakuwa mwongozo mzima wa mada yetu kwa siku ya leo.
NJIA SAHIHI YA KUMJUA MWENYEZI MUNGU
Inawezekana kukawa na njia mbalimbali
katika kujibu swali hili, lakini hatutakuwa na njia ambayo ni bora zaidi kwetu,
kama kumtambua Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwake mwenyewe. Na hapa kwetu sisi
kama Waislamu hatutakuwa na marejeo zaidi ya kurejea katika maneno yake
matakatifu ambayo kama kutakuwa na njia nyingine basi yeye mwenyewe atatuelekeza.
Lakini katika jambo hili, kunaweza kukawa
na mswali mawili matatu ambayo tunaweza kujiuliza, kama ambavyo ni lazima pia
yaweze kupatiwa ufumbuzi sahihi. Moja ya maswali hayo ni kwamba, je Quran imeelezea juu ya uwepo wa
Mwenyezi Mungu, mpaka sisi kupia Quran tuweze kusema kuwa tumegundua uwepo wake
na hatimaye tuweze kutambua sifa zake?.
Katika kujibu swali hili, kuna rai mbili
ambazo tunaweza kuzileta hapa, na kisha kuweza kubainisha rai sahihi kuhusiana
na swali husika.
Itaendelea......