bayyinaat

Published time: 05 ,February ,2017      19:18:35
Kila sifa njema basi inamstahiki Mwenyezi Mungu, ambaye ana kila haki ya kusifika na sifa njema pasi na mwingine asiyekuwa yeye. Kwani hakuna jambo ambalo utaweza kulizungumzia ila utakuta ndani yake kuna kila sababu ya kuweza kumtaja na kumtukuza yeye katika jambo hilo.
News ID: 7

Pia sala, salamu na amani ziende moja kwa moja kwa mtukufu wa cheo na daraja, Mtume Muhammad (saww) pamoja na kizazi chake ambacho kimetakaswa utakaso ulio kamili.

Napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha ewe ndugu msomaji, katika uwanja huu wa makala za kielimu juu ya maisha yetu kwa ujumla, kuanzia ngazi ya hapa duniani mpaka kesho siku ya kiyama. Lengo likiwa ni namna moja ama nyingine kuweza kufikishiana yale ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku, huku tukiwa tumelenga na kuangalia nyanja zote mbili za maisha y mwanadamu.

Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu katika uwanja huu, tutakuwa tukichambua na kupashana mambo yote yanayohusiana na maswala ya itikadi katika dini yetu ya Kiislamu, tukianzia katika swala zima la kumpwekesha Mwenyezi Mungu (Tawhid) mpaka swala zima la ufufuo wa siku ya mwisho (kiyama).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe ni wenye kunufaika na kunufaisha wengine kwa haya ambayo tunakwenda kuchambua katika uwanja huu, na hatimaye tuwe ni katika ambao wamesimama kwa namna moja au nyingine katika kuiendeleza dini yake Mwenyezi Mungu aliye mtukufu.

Mwandishi

Sheikh Abdulrazak Rashid Bilal


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: