bayyinaat

Published time: 24 ,February ,2017      19:06:26
Ndio ni wajibu wa Mwanamke aliyeolewa kuomba idhini kwa mumewe ya kutoka nje ya nyumba, na falsafa yake pia iko wazi.......
News ID: 20

baadhi ya misimamo kwa Mwanamke

Swali:

Uislamu hakutofautisha katika kuwaagiza kidini kati ya wanaume na wanawake, wote wawili wako sawa katika matilaba kuhusu kumuabudu Mungu, kusimamisha Dini yake na kulingania watu kumuelekea Allah, kuamrisha mema na kukemea mabaya.

Aidha Quran imembebesha Mwanamume na Mwanamke majukumu ya kusimamia masilahi ya jamii na kuurekebisha kwa maana kwamba kuamrisha mema na kukemea mabaya  katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

(وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ).

"Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humtii  Mwenyezi Mungu na Mtume wake”. Tawbah; 71.

Hivyo wanawake wameshiriki katika zama za Mtume Muhammad, na zama za makhalifa katika nyanja mbalimbali za maisha, na mielekeo mbalimbali hata katika hatua za kufikisha Ujumbe wa uanzishwaji wa dola ya Kiislam, hivyo duru ya Mwanamke ilikuwa pana zaidi kuliko wanaume.
Hivyo kwa nini baadhi ya Maulama wa Kiislamu husisitiza zaidi juu ya misimamo dhidi ya wanawake, itakayozuia haki zao za msingi hata wakati wa kutoka nyumbani, na wakati mwingine kuwazuia kujifunza, na wakati mwingine kuwazuia kushiriki katika maisha ya kisiasa, wapi hutokea tatizo?
Ni ukosefu wa uwazi wa maandiko ya sheria ya Qur'an na Sunna au katika mila na desturi ambazo ya sababu ya udhalimu wao na chuki dhidi ya wanawake au katika utamaduni wa kileo na sera za kubomolewa matukufu yao, je! Si sababu ya mlango wao kufungwa na kuwashambulia kisaikolojia na mwelekeo binafsi na kulazimisha wengine kutohusika kufanya kazi zao za nje?

Jawabu:

Uislamu katu haukumzuia Mwanamke asiende nje ya nyumba na kujifunza na kutoshiriki katika maisha ya kisiasa wakati wote.

Ndio ni wajibu wa Mwanamke aliyeolewa kuomba idhini kwa mumewe ya kutoka nje ya nyumba, na falsafa yake pia iko wazi, kwani matakwa ya maisha ya Mke Uislamu umeyaweka mikononi mwa Mume, amesema Allah:

(الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ)

"Wanaume ni wasimamizi wa wanawake”.

Na sababu ya hayo ni kwa kuwa Mwanamume ni mwenye uwezo wa matakwa kuliko Mwanamke, hii ni ya kwanza.

Ya pili: Ni kwa sababu Mwanamume ni mfadhili wa maisha ya Mke, aidha ni kawaida kiongozi yapaswa awe ni mtu mwenye uwezo wa matakwa na mfadhili hodari ambaye atatimiza na kumlea Mwanamke na kumpa kila hitaji lililokuwa ndani ya uwezo wake, chunguza  Zaidi katika Aya tukufu:

(الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ).

"Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa”.

Hivyo ikiwa utashi kamili uko mikononi mwa Mwanamume, basi ni kawaida (Mwanamke) asitoke nje ya nyumba bila idhini ya kiongozi, iko wapi hii ya kusema Uislamu umemzuia Mwanamke kutoka nje ya nyumba?

 

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: