bayyinaat

Published time: 28 ,May ,2017      13:37:25
Kwa hakika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi ambao unakuja kwa lengo la kumjenga mwanadamu na kumjulisha ya kwamba swala la kuambatana na muumba wake si swala la wakati maalumu pasi na wakati mwingine.....
News ID: 93دعاء اليوم الحادي عشر

Dua siku ya kumi na moja


اَللّهُمَّ حَبِّبْ اِلَيَّ فيهِ الْإحسانَ ، وَ كَرِّهْ فيهِ الْفُسُوقَ وَ العِصيانَ وَ حَرِّمْ عَلَيَّ فيهِ السَخَطَ وَ النّيرانَ بعَوْنِكَ ياغياثَ المُستَغيثينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nifanye katika siku hii niupende wema, na nichukie uovu na uasi, na niharamishie chuki na hasira za moto, kwa haki ya msaada wako ewe msaidizi wa wenye kuomba msaada”.دعاء اليوم الثاني عشر

Dua siku ya kumi na mbiliاَللّهُمَّ زَيِّنِّي فيهِ بالسِّترِ وَ الْعَفافِ ، وَ اسْتُرني فيهِ بِلِباسِ الْقُنُوعِ و َالكَفافِ ، وَ احْمِلني فيهِ عَلَى الْعَدْلِ وَ الْإنصافِ ، وَ آمنِّي فيهِ مِنْ كُلِّ ما اَخافُ بِعِصْمَتِكَ ياعصمَةَ الْخائفينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nipambe kwa sitara na kujizuia, na unipambe na vazi la kutosheka, na uniweke katika uadilifu na usawa, na unipe amani kutokana na kila ninaloliogopa, kwa haki ya hifadhi yako ewe muhifadhi wa wenye kuogopa”.دعاء اليوم الثالث عشر

Dua siku ya kumi na tatuاَللّهُمَّ طَهِّرْني فيهِ مِنَ الدَّنسِ وَ الْأقْذارِ ، وَ صَبِّرْني فيهِ عَلى كائِناتِ الْأَقدارِ ، وَ وَفِّقْني فيهِ لِلتُّقى وَ صُحْبَةِ الْأبرارِ بِعَوْنِكَ ياقُرَّةَ عَيْن الْمَساكينِ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii naomba unitakase kutokana na uchafu na mabaya, na unipe subira kutokana na mipango ya kadari, na unijaalie uchamungu na kuongea yaliyo mema, kwa haki ya msaada wako ewe pozo la wenye haja”.دعاء اليوم الرابع عشر

Dua siku ya kumi na nneاَللّهُمَّ لاتُؤاخِذْني فيهِ بالْعَثَراتِ ، وَ اَقِلْني فيهِ مِنَ الْخَطايا وَ الْهَفَواتِ ، وَ لا تَجْعَلْني فيهِ غَرَضاً لِلْبَلايا وَ الأفاتِ بِعزَّتِكَ ياعِزَّ المُسْلمينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii usinihukumu katika ambayo nimeteleza, na uniepushe kutokana na makosa na kuteleza, na wala usinifanye kuwa sehemu ya mabalaa na maangamio, kwa haki ya utukufu wako ewe mwenye kuwatukuza Waislamu”.دعاء اليوم الخامس عشر

Dua siku ya kumi na tanoاَللّهُمَّ ارْزُقْني فيهِ طاعةَ الخاشعينَ ، وَ اشْرَحْ فيهِ صَدري بِانابَةِ المُخْبِتينَ ، بِأمانِكَ ياأمانَ الخائفينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie katika siku hii utiifu wa wenye kukuogopa, na ukifungue kifua changu niweze kukuelekea mwelekeo wa wenye imani kwako, kwa haki ya amani yako ewe amani ya wenye hofu”.دعاء اليوم السادس عشر

Dua siku ya kumi na sitaاَللّهُمَّ وَفِّقْني فيهِ لِمُوافَقَةِ الْأبرارِ ، وَ جَنِّبْني فيهِ مُرافَقَةِ الأشرارِ ، وَآوني فيهِ برَحمَتِكَ إلى دارِ القَرارِ بإلهيَّتِكَ يا إله العالمينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nijaalie niwe ni mwenye kuambatana na watu wema, na niepushe na kuambatana na waovu, na uniweke kwa rehema zako katika nyumba ya milele, kwa haki ya uungu wako ewe mola wa walimwengu”.دعاء اليوم السابع عشر

Dua siku ya kumi na saba


اَللّهُمَّ اهدِني فيهِ لِصالِحِ الأعْمالِ ، وَ اقضِ لي فيهِ الحوائِجَ وَ الآمالِ يا مَنْ لا يَحتاجُ إلى التَّفسيرِ وَ السُّؤالِ ، يا عالِماً بِما في صُدُورِ العالمينَ صَلِّ عَلى مُحَمَّدٍ وَ آله الطّاهرينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, niongoze katika siku hii kuelekea matendo bora, na unitimizie haja zangu na matarajio yangu, ewe ambaye hahitaji kuelezewa wala kuulizwa, ewe mjuzi wa yaliyo katika nyoyo za walimwengu, mswalie mtume Muhammad saww pamoja na kizazi chake kilichotakasika”.دعاء اليوم الثامن عشر

Dua siku ya kumi na nane


اَللّهُمَّ نَبِّهني فيهِ لِبَرَكاتِ أسحارِهِ ، وَ نوِّرْ قَلْبي بِضِياءِ أنوارِهِ ، وَ خُذْ بِكُلِّ أعْضائِي إلى اتِّباعِ آثارِهِ بِنُورِكَ يا مُنَوِّرَ قُلُوبِ العارفينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii naomba unizindue kwa ajili ya baraka za usiku wake, na ung’arishe moyo wangu kwa nuru zake, na ufanye nguvu zangu zote ziwe ni zenye kufuata athari zake, kwa haki ya nuru yako ewe mng’arishaji wa nyoyo za wenye kukujua”.دعاء اليوم التاسع عشر

Dua siku ya kumi na tisa


أللّهُمَّ وَفِّر فيهِ حَظّي مِن بَرَكاتِهِ ، وَ سَهِّلْ سَبيلي إلى خيْراتِهِ ، وَ لا تَحْرِمْني قَبُولَ حَسَناتِهِ يا هادِياً إلى الحَقِّ المُبينِ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nitimizie hadhi yangu kutoka katika baraka zako, na ujirahisishie njia ya kuelekea heri zake, na wala usininyime haki ya kukubaliwa mema yake, ewe mwongozaji kuelekea njia ya haki”.دعاء اليوم العشرين

Dua siku ya ishiriniأللّهُمَّ افْتَحْ لي فيهِ أبوابَ الجِنان ، وَ أغلِقْ عَنَّي فيهِ أبوابَ النِّيرانِ ، وَ وَفِّقْني فيهِ لِتِلاوَةِ القُرانِ يامُنْزِلَ السَّكينَةِ في قُلُوبِ المؤمنين

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nifungulie milango ya pepo, na unifungie milango ya moto, na unijaalie nisome Quran, ewe mwenye kuteremsha utulivu katika nyoyo za waumini”.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: