bayyinaat

Published time: 28 ,May ,2017      13:43:31
ili mradi tu mwanadamu asiwe ni mwenye kujisahau ya kwamba anatakiwa daima awe ni mwenye kushikamana na mola wake, na mfano wa dua hizo ni dua ambazo kila siku Mwislamu anatakiwa asome katika........
News ID: 94



دعاء اليوم الحادي والعشرين

Dua siku ya ishirini na moja



أللّهُمَّ اجْعَلْ لي فيهِ إلى مَرضاتكَ دَليلاً ، و لا تَجعَلْ لِلشَّيْطانِ فيهِ عَلَيَّ سَبيلاً ، وَ اجْعَلِ الجَنَّةَ لي مَنْزِلاً وَ مَقيلاً ، يا قاضِيَ حَوائج الطالبينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nitengenezee njia ya kuelekea ridhaa zako, na wala usimpe shetani njia ya kunifikia, na ifanye pepo kuwa ndio mafikio na makazi yangu, ewe mtekelezaji wa haja ya wenye kumuomba”.



دعاء اليوم الثاني و العشرين

Dua siku ya ishirini na mbili


أللّهُمَّ افْتَحْ لي فيهِ أبوابَ فَضْلِكَ ، وَ أنزِل عَلَيَّ فيهِ بَرَكاتِكَ ، وَ وَفِّقْني فيهِ لِمُوجِباتِ مَرضاتِكَ ، وَ أسْكِنِّي فيهِ بُحْبُوحاتِ جَنّاتَكَ ، يا مَجيبَ دَعوَةِ المُضْطَرِّينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nifungulie katika siku hii milango ya fadhila zako, na unishushie baraka zako, na uniwafikishe kwa ajili ya ambayo ni sababu ya ridhaa yako, na uniweke katika pepo yako, ewe mwenye kujibu dua na maombi ya wenye matatizo”.



دعاء اليوم الثالث و العشرين

Dua siku ya ishirini na tatu


أللّهُمَّ اغْسِلني فيهِ مِنَ الذُّنُوبِ ، وَ طَهِّرْني فيهِ مِنَ العُيُوبِ ، وَ امْتَحِنْ قَلبي فيهِ بِتَقْوى القُلُوبِ ، يامُقيلَ عَثَراتِ المُذنبين

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nisafishe kutokana na madhambi, na uniondolee aibu, na moyo wangu uupe mtihani kwa ajili ya kukucha , ewe msamehevu wa makosa ya wenye makosa”.



دعاء اليوم الرابع و العشرين

Dua siku ya ishirini na nne


أللّهُمَّ إنِّي أسألُكَ فيهِ مايُرضيكَ ، وَ أعُوذُ بِكَ مِمّا يُؤذيكَ ، وَ أسألُكَ التَّوفيقَ فيهِ لِأَنْ اُطيعَكَ وَلا أعْصِيَكَ ، يا جواد السّائلينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, hakika katika siku hii nakuomba yale ambayo yanakuridhisha, na najikinga kwako kutokana na yanayokuudhi, na nakuomba tawfiq ya kuweza kukutii bila ya kukuasi, ewe mkarimu kwa wenye kumuomba”.



دعاء اليوم الخامس و العشرين

Dua siku ya ishirini na tano


أللّهُمَّ اجْعَلني فيهِ مُحِبّاً لِأوْليائكَ ، وَ مُعادِياً لِأعْدائِكَ ، مُسْتَنّاً بِسُنَّةِ خاتمِ أنبيائكَ ، يا عاصمَ قٌلٌوب النَّبيّينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie katika siku hii niwe ni mwenye kuwapenda vipenzi vyako, na ni mwenye kuwachukia maadui zako, niwe ni mwenye kushikamana na mienendo ya mbora wa mitume wako (Muhammad saww), ewe mlinzi wa nyoyo za mitume”.



دعاء اليوم السادس و العشرين

Dua siku ya ishirini na sita



أللّهُمَّ اجْعَلْ سَعْيي فيهِ مَشكوراً ، وَ ذَنبي فيهِ مَغفُوراً ، وَ عَمَلي فيهِ مَقبُولاً ، وَ عَيْببي فيهِ مَستوراً يا أسمَعَ السّامعينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, naomba katika siku hii ufanye juhudi zangu ni zenye kushukuriwa, na dhambi zangu ziwe ni zenye kusamehewa, na matendo yangu yawe ni yenye kukubaliwa, na aibu zangu ziwe ni zenye kusitirika, ewe mbora wa wasikivu wote”.



دعاء اليوم السابع و العشرين

Dua siku ya ishirini na saba


أللّهُمَّ ارْزُقني فيهِ فَضْلَ لَيلَةِ القَدرِ ، وَ صَيِّرْ اُمُوري فيهِ مِنَ العُسرِ إلى اليُسرِ ، وَ اقبَلْ مَعاذيري وَ حُطَّ عَنِّي الذَّنب وَ الوِزْرَ ، يا رَؤُفاً بِعِبادِهِ الصّالحينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, nijaalie katika siku hii fadhila za usiku wa cheo (Lailatul Qadr), na uyabadili mambo yangu kutoka katika ugumu kwenda katika wepesi, na nikubalie udhuru zangu, na unitue madhambi na izigo yangu, ewe mpole kwa waja wake”.



دعاء اليوم الثامن و العشرين

Dua siku ya ishirini na nane


أللّهُمَّ وَفِّرْ حَظِّي فيهِ مِنَ النَّوافِلِ ، وَ أكْرِمني فيهِ بِإحضارِ المَسائِلِ ، وَ قَرِّبْ فيهِ وَسيلَتي إليكَ مِنْ بَيْنِ الوَسائِلِ ، يا مَن لا يَشْغَلُهُ إلحاحُ المُلِحِّينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nipatie hadhi ya kutimiza suna zake, na unikirimu kwa kutimiza ya muhimu, na ifanye karibu njia yangu ya kukuelekea wewe, ewe ambaye uharaka wa wenye haraka wala haumshughulishi”.



دعاء اليوم التاسع و العشرين

Dua siku ya ishirini na tisa


أللّهُمَّ غَشِّني فيهِ بالرَّحْمَةِ ، وَ ارْزُقني فيهِ التَّوفيقَ وَ العِصْمَةَ ، وَ طَهِّر قَلبي مِن غياهِبِ التُّهمَةِ ، يارَحيماً بِعبادِهِ المُؤمنينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii nifunike na rehema zako, na uniruzuku tawfiq na nguvu ya kujikinga, na usafishe moyo wangu kutokana na giza, ewe mpole kwa waja wake waumini”.



دعاء اليوم الثلاثين

Dua siku ya thelathini


أللّهُمَّ اجْعَلْ صِيامي فيهِ بالشُّكرِ وَ القَبولِ عَلى ما تَرضاهُ وَ يَرضاهُ الرَّسولُ مُحكَمَةً فُرُوعُهُ بِالأُصُولِ ، بِحَقِّ سَيِّدِنا مُحَمَّدٍ وَآلهِ الطّاهِرينَ ، وَ الحَمدُ للهِ رَبِّ العالمينَ

"Ewe Mwenyezi Mungu, katika siku hii naomba uifanye saumu yangu iwe ni yenye kushukuriwa na kukubaliwa nawe kwa yale ambayo unayaridhia wewe pamoja na Mtume wako saww, na iwe ni yenye kuimarika misingi yake, kwa haki ya mtukufu Mtume Muhammad saww na kizazi chake kilicho chema, na sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu mola wa walimwengu”.

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: