bayyinaat

Published time: 04 ,October ,2017      20:47:05
Imam (a.s) alipoona maovu yanafanyika hadharani kwa jina la Mtume (s.a.w.w) na watu kuanza kuushakia Uislamu kutokana na mambo wanayo yafanya madhalimu waliojitambulisha.........
News ID: 98

MATUNDA YA SHAHADA YA IMAMHUSEIN(As)

Sifa zote njema ni zake mwenyezi mungu mola wa walimwengu wote, rehema na amani zimuendee Mtume Muhammad( s.a.w.w) na kizazi chake hasa mjukuu wake Imam Husein (a.s)

Hakika majilisi zote zinazofanyika kwaajili ya kuomboleza kifo cha Imam Husein (a.s) katika mwezi wa Muharamu ni miongoni mwa mambo muhimu yanayo watofautisha mashia na Waislamu wengine.

Kuhuisha Ashura ni jambo lenye fadhila kubwa sana katika dini, na Haifai kudhania kwamba suala la kulia katika Muharamu ni desturi za watu wa zamani zisizofaa kuwepo katika ulimwengu huu wa Mantiki na. Fikra hizo hazifai, na nibatili kwa sababu kila kitu kina sehemu yake, kwani Mungu alipo muumba mwanadamu alimpa Akili, hisia za huzuni na furaha, na kila kimoja kinanafasi yake katika kumkamilisha mwanadamu na kujenga utuwake. Hivyo basi tunasema kwamba hisia za kimaumbile alizonazo mwanadamu zina nafasi yake kimantiki, na kuna mambo mengi ambayo hayapatikani ufumbuzi wake kwa kutumia Mantiki na Dalili, bali hutatuka kwa kuamsha hisia zinazooana na jambo husika. Na historia ya Mitume wote waliofanikiwa kuwaingiza watu katika Dini ya Mungu ilikua si kwakutumia Mantiki na Dalili tu, bali kwa kuamsha hisia zao pia zilikuwa mojawapo ya njia za ulenganiaji wao.

MAANA YA ASHURAA

ASHURAA: Imepokelewa katika Lisanul arab kwamba: neno Ashuraa litamkwapo humaanisha siku ya kumi ya Muharamu. Ama baada ya kutokea tukio la kuuwawa imamu Husein (a.s) na hasa katika zama hizi neno hili limekua likitumika kwamaana; kumi la kwanza la mwezi wa Muharram, ambapo huwekwa Majilisi mbalimbali kwaajili ya kuomboleza kifo cha Imam Husein. Na ukweli ni kwamba Ashuraa ni mfumo wa kijamii ulio hai daima unao lazimisha kuigeuza sehemu yeyote inayo tendeka Dhulma na Uovu kua ni Karbala, nazama zote ambazo zitaenea maovu kua ni Ashuraa.

SABABU ZA MAPINDUZI YA IMAM HUSEIN (a.s)

Mambo ambayo yalipelekea Imam kufanya mapinduzi na hatimaye kufa kishahidi yalikuwa kama ifuatavyo:

1-Watawala wa zama hizo walikusudia kuuangamiza Uislamu.

Yazidi alikuwa ni mtu asie uamini Uislamu tokea hapo kabla bali alikua amebeba uadui mkubwa dhidi ya Uislamu moyoni mwake

2-Kuandaliwa mikakati ya kutaka kuudidimiza Uislamu

Shahada ya imamu Husein na maadui wa Uislamu chini ya utawala haram wa baniumayyah.

3-Siasa za utawala wa Yazidi katika utendaji wake ni kutaka kufuta na kupoteza juhudi za Mtume (s.a.w.w)

Yazidi alikusudia kuufuta Uislamu na kupoteza juhudi za mtume pia juhudi za Waislamu waliotoa Damu zao na nafsi zao kwa ajili ya kutetea Dini ya haki wasibakiwe na utajo katika duniani.

4-Kupotosha mafundisho ya Kiislamu

Utawala wa Muawiah haukuwa na lengo zaidi ya kupotosha mafunzo ya Kiislamu na kubomoa misingi ya dini kama vile kuasisi kuwatusi Masahaba wa mtukufu Mtume (s.a.w.w).

5-Kuuarifisha Uislamu vi mbaya na kuugeuza uhakika wake

Walikusudia baniumayyah kudhihirisha uislam kwa matendo ya watawala waovu na kuchafua utajo wa mtume (s.a.w.w) nawatawala hao waliyafanya mambo machafu ambayo hajawahi kuyafanya mtawala yeyote baada yao.

6-Mapinduzi ya Imam Husein (a.s) ilikuwa ni kusimama dhidi ya utawala wa madhalimu.

Baniumayyah waliugeuza utawala wa Kiislamu kua ni ufalme na kuyapiga vita mafunzo ya kiroho yanayomtukuza Mwanadamu.

7-Kuukosea adabu Uislamu na sheria zake .

Imam (a.s) alipoona maovu yanafanyika hadharani kwa jina la Mtume (s.a.w.w) na watu kuanza kuushakia Uislamu kutokana na mambo wanayo yafanya madhalimu waliojitambulisha kama viongozi wa Kiislam.

MALENGO YA MAPINDUZI YA IMAM HUSEIN

1-Kuhuisha Uislamu na kuokoa kutoka mikononi mwa Madhalimu

Muharamu ni mwezi ambao Imam Husein (a.s) aliuhuisha Uislamu na kuokoa kutokana na vitimbi vya Madhalimu.

2-Kuuhifadhi mustakabali wa Uislamu na Waislamu

Imam Husein (a.s) alifikiria mustakabali wa Uislamu na Waislamu kwani alilewa kwamba shahada yake itapelekea kuenea Uislamu ulimwenguni na kwamba mfumo wa mapinduzi yake utabakia kuwa ni funzo katika jamii zetu.

3-Kuondoa Khofu katika nyoyo za Waislamu na watu wote.

woga na Khofu ni suala ambalo lilikuwa limeenea katika nyoyo za watu kwa kiwango kikubwa, kiasi kwamba hakuna yeyote alikuwa anaweza kuthubutu kuongea hata neno moja dhidi ya watawala wa zama hizo, kwa ajili hiyo watu wakawa hawana budi kusalimu amri kwenye utawala dhalimu, hivyo kutokana na mazingira hayo kukawa na ulazima ajitokeze mtu atakayepambana na madhalimu hawa kwaajili ya kuwarejeshea watu roho ya ushujaa na mashambulizi ambae ni Imam Husein (as).

4-Kutengeneza Umma na kutokomeza serikali ya waovu

Wote wanao mtawalisha Imam Husein (a.s) wanapaswa kudurusu kwa makini tukio la Karbala na kuchukua Ibra na mazingatio. japokuwa Imam alikua na watu wa chache, na yazidi alikuwa na jeshi kubwa lakini yeye ndie aliyeshinda, hivyo basi msiogope kufanya mambo yenu kwa uchache wa idadi yenu.


LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: