bayyinaat

Published time: 04 ,October ,2017      20:54:17
Kama si mapinduzi ya Imam Husein (a.s) Uislamu usingetufikia salama, kwani yazidi na jopo lake walikuwa wamekusudia kuharibu........
News ID: 99

MATUNDA YASHAHADA YA IMAM HUSSEIN(AS)

A- Uislamu umehifadhika na kubaki kwa baraka za mapinduzi yake

Kama si mapinduzi ya Imam Husein (a.s) Uislamu usingetufikia salama, kwani yazidi na jopo lake walikuwa wamekusudia kuharibu Uislamu na kuumaliza moja kwa moja

B- Uislamu kuhuika kwa Muharram.

Shahada ya Imam Husein (a.s) katika siku ya Ashuraa imepelekea Uislamu kuhuika na kuchukua sura mpya kila unapofika mwezi wa Muharamu, na watu kuufanya mwezi huo kua ndio mwezi wa kuhuisha Uislamu , kiasi kwamba mpaka leo imebaki kuwa ndio athari kubwa ya Shahada ya Imam Husein(a).

C- Shahada ya Imam (a.s) imezuia kurejea zama za Ujahili na Ukafiri

Laiti kama si Imam Husein (a.s) kujitoa muhanga, yazidi pamoja na Madhalimu wenzake walikuwa tayari wamekusudia kuipa nguvu nidhamu ya kidhalimu nakurejesha mazingira yaliyokuwepo zama za ujahili. Na mfano juu ya hilo nipale Yazidi alipo halalisha maovu katika mji wa Madina na kuibomoa Kaaba ambayo hata mshirikina zama za ujahili walikuwa wanaiheshimu. Hivyo basi laukama si mapinduzi ya Imam Husein (a.s) Uislamu tulionao ungekua kama wa Yazidi kutokana na mikakati aliokuwa dhidi ya Uislamu. Kwa sababu hiyo ndio maana ya usemi huu kwamba Imam Husein (a) kaukomboa Uislamu na umma.

D- Mapinduzi ya Imam (a.s) yamewapa kutetea haki na kuto ogopa chochote

Tumejifunza katika shahada ya Imam Husein(a.s) na Ahali zake na masahaba wake kwamba wanawake na wanaume wote kwa ujumla hawatakiwi kuogopa kuishambulia Dhulma na madhalimu.

E- Kuhifadhi Qur`an na juhudi za Mtume (s.a.w.w)

Madhalimu wa zama hizo walikua wamekusudia kupoteza juhudi alizozifanya Mtume (s.a.w.w)katika kuujenga umma, kama vile walivyokusudia kufuta Athari za Uislamu alizoziacha Mtume (s.a.w.w), na Athari hizo ni kama vile Qur`ani na mengineyo. Lakini mapinduzi ya Imam Husein (a.s) yaliwafanya wafeli katika malengo yao. Na mkakati huo ulikuwa ni wa muda mrefu ambao ulikuwepo pia hata katika zama za Mtume (s.a.w.w), na kinara wa mkakati huo ni babu yake yazidi aitwae kwa jina la Abu Sufian, na Yazidi alirithi kutoka kwa baba yake na babu yake, na ndio maana alikuwa akinadi hadharani na kusema hakuna habari yoyote wala Wahy ulioshuka kutoka mbinguni.

F- Kubainisha wadhifa , mafunzo sahihi ya kulingania

Imam Husein (a.s) alijitoa muhanga wakati ambao watu walikuwa hawaelewi wadhifa wao dhidi ya utawala wa Yazidi ni nini?, lakini mapinduzi ya Imam (a.s) na masahaba wake yaliwafanya waelewe kwamba wadhifa wao ni kutetea haki.

***


LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: