bayyinaat

Published time: 13 ,February ,2017      22:37:55
Nini mtazamo Kiislamu juu ya haki za kifamilia? Je! Kuongeza wake ni mtaala unaotegemea uhakika wa uadilifu wao?
News ID: 16
Je! wake wengi ni mtaala unaotegemea uhakika wa uadilifu kati yao?

Swali:

Nini mtazamo Kiislamu juu ya haki za kifamilia? Je! Kuongeza wake ni mtaala unaotegemea uhakika wa uadilifu wao?

Jawabu:

Ndiyo, Hakika hayo hutegemea uaminifu wa mtu mwenyewe kufikia uadilifu baina ya wakeze.

Anasema Mwenyezi Mungu katika Surat Anisaai: 3:

(وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً).

"Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu”.

Hakika wanachuoni wetu wameeleza kwa ubainifu zaidi katika vitabu vya kifiqhi na risala za matendo uadilifu huu wa kifamilia, na namna Mume apaswa kusimamia uadilifu baina ya wakeze, na kwa ibara dhahiri ya matilaba haya, ni kumpa kila mmoja haki yake na kugawa uadilifu kwa kila anayestahiki bila kupoteza haki ya kila mmoja miongoni mwao.
Ama uadilifu chanya katika kauli yake Mwenyezi Mungu:
(وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ).
"Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia”. An-nisaai; 129.
Imefasiriwa ni; Uadilifu katika upendo na kupendelea moyo kuelekea kwao, kwani Mtu kawaida hawezi kuleta wala kujenga usawa kati yao katika suala zima la upendo, lakini ni kawaida kwa Mwanamume kuongeza upendo kwa baadhi yao, hivyo ni wajibu wa mume kufanya uadilifu pindi anapoonesha upendo na mwelekeo kwa baadhi yao, lakini pamoja na hivyo hapaswi kuelekeza upendo kwa baadhi na kuacha wengine kama walio tundikwa, hajawekewa akiba wala kuruhusiwa kuweza kuoa mke mwingine kwa tabia ya namna hiyo, kama asemavyo Allah:
(فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ).
"Kwa hivyo msielekee moja kwa moja kwa mmoja wao na mkamwacha (mmoja) kama aliye tundikwa (hana kazi wala faida)”. An-nisaai; 129.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: