KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA NA MWENYE
KUREHEMU
Mtukufu mtume (s.a.w.w):
«إذا صلت المرأة خمسها و صامت شهرها و أحصنت فرجها
و أطاعت بعلها فلتدخل من أي أبواب الجنة شاءت».
"Atakaposali Mwanamke Sala zake tano, na
akafunga mwezi wake mtukufu, na akalinda tupu yake, na akamtii Mumewe basi
ataingia peponi kupitia mlango apendapo”.
Mke mwema ni hazina (yenye thamani) ya Muumini:
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbas kuwa amesema:
Iliposhuka Aya hii
(...والذين يكنزون الذهب والفضة...).
"…Na ambao hukusanya dhahabu na fedha…”.
Thuban alimjia Mtume (s.a.w.w) akamuuliza: Ewe
Mjumbe wa Allah; Kushuka Aya hii, ni kwa sababu ya kiburi cha Masahaba wako?
Akasema (s.a.w.w): "Je! Nikueleze ni ipi hazina bora? Akasema (s.a.w.w): Ni mke
mwema, ambae mumewe akimuangalia hufurahi, na akimuamuru humtii (humsikiliza),
na asipokuwa naye basi humlinda”.
Utiifu wa Mke kwa mumewe sawa iwe kwa siri au
dhahiri ni faradhi ambayo haihitajii mkataba za ndoa, na ikiwa Mke atakataa
kumtii Mumewe basi itapekea mume kuwa mkaidi, na kuzuka mikingamo ya kifamilia,
na kila atakapozidi kumtii ndipo mapenzi yatazidi baina yao, na hiyo itahamia
kwa watoto wao, Hakika tabia zenye kupendana huwa ni chimbuko la kuhamia kwa
watoto, wakiume kurithi kutoka kwa baba zao, na wa kike kurithi kutoka kwa Mama
zao, kwani Mtume (s.a.w.w) amemhimiza sana Mwanamke kumtii mumewe, akasema:
Mambo matatu hayapatwi na moto wa Jahanamu siku ya kiama: " mwanamke anayemtii
Mumewe, na Mtoto mwema kwa Wazazi wake wawili, na Mja ambaye ni hakimu wa kweli
kwa haki ya Mungu wake na Mkuu wake”.
Akasema tena (s.a.w.w): "Jihadi ya Mwanamke ni
kuwa mke bora kwa Mumewe”. Hakika utiifu pasi na muamala mwema hautoshi, kwa
Sababu Mwanamke anaweza kumtii mumewe na asiwe mwenye tabia njema kwake.
Akafanya aambiwayo, na asifuatilie hatma yake, ambapo kwamba; Mwendo mzuri ni
kumtii akitakacho mume, na kudhihirisha mapenzi ya kweli katika hilo, na
kumuonesha mumewe tabasamu na bashasha ya kuridhika na matakwa yake, na
kumsikilizisha maneno matamu, Hakika Mke kufanyia hayo basi humtuliza Mume na
kumpoza roho yake.
Na yampasa Mwanamke kuzingatia nini maana ya
utiifu kiukamilifu, kwani utiifu huo ndio hupelekea Mwanamke kumiliki moyo wa
Mumewe, na kuchuma uaminifu wake, na kudumisha mapenzi yake, akifanya hivyo
basi Mume atamkabili Mkewe kama vile Yeye ndiye anayemtii mke, na kujali
apendayo Mkewe.
Hakika ni wanawake wachache ndio wanaofahamu
jambo hilo, pia ni wachache ndio wanaolifanyia kazi suala hilo, hapana shaka ya kwamba:
Utiifu ndio unaokuza Shina za mapenzi baina ya wanandoa wawili, na pindi Mke
atampenda mumewe kwa dhati basi hapana budi kumtimizia haki zake zote za
kimsingi, yote hiyo ni picha ya matendo na alama za Mume za mapenzi
zinazosababisha kutuliza moyo wake.
Minajili hiyo Mtume anasema: "Hakika Dunia ni
starehe na starehe yake bora mno ni Mke mwema, utakapomuangalia (mkeo)
hufurahishwa naye, na utakapomuamuru basi hukutii, na utakapomuapia hukufahamu,
na ukiwa mbali naye hukulindia heshima yako na mali yako”.
Hakika huyo ni Mke mwema, mwenye upendo wa
kweli, humtabasamia mumewe pindi anapomtazama kiasi kwamba mume kushindwa
kuangalia mwingine zaidi yake, na wala macho ya wengine hayambabaishi maadamu
yuko mwenye kumfurahisha kwa mapenzi na bashasha.
Miongoni mwa utiifu wa Mke kwa mume, ni Mke
kutofunga ila kwa idhini ya mumewe, asitoke ila kwa idhini yake, asilete yeyote
nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe na asitumie mali yake ila kwa idhini
yake, aishi pamoja na Mume kwake, na hii katika njia ya mifano iliyo wazi.
Hakika Mwanamke hawezi kutimiza haki ya Mola
wake mpaka atimize ya Mumewe, na muhimu zaidi ni utiifu. Amesema Mtukufu Mtume (s.a.w.w): "Watu watatu
hazikubaliki Sala zao, wala hazipandi mbinguni amali zao njema” akata moja wapo
kuwa: Mke kukasirikiwa na Mumewe hadi atakapomridhisha Mumewe.