Historia
Mtume (s.a.w.w)
MWANZO WA MAZUNGUMZO:
Maisha ya jamii sio matokeo tofauti yasiyokuwa na uhusiano wowote, lakini ni endelezo,
linalochukua yote yaliyopita katika juhudi zake za kila siku na mapambano endelevu na kuyaweka
katika zama za sasa hivi, ili kupata kutoka kwake nguvu inayoitegemewa pamoja na harakati, na
nyenzo za maendeleo yake, kisha maendeleo yake yaendelee katika hatua thabiti na tulivu
kuelekea mustakbal anaoutamani na anaoutaka.